Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- POLISI NA WANAHABARI MBEYA WAWEKA MIPANGO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
- Yamenifika makubwa baada ya kuikataa mimba yake
- Happy birthday Dr. Tulia
- Viongozi 11 wa CHADEMA washikiliwa na Polisi Mkoa wa Songwe
- ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAHUNDI ZANZIBAR
- Jinsi ya Kufikisha Malalamiko Kuhusu Mradi wa REGROW na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
- Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi Akagua Hali ya Mawasiliano Kisiwani Kojani, Pemba
- Inauma sana: Mtoto wangu kaenda chuo kikukuu katumbukia katika umalaya na dawa za kulevya
Author: Mbeya Yetu
Mashauri matatu yalizofunguliwa Mahakama ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya kwa Hati ya dharula na Aidan Msigwa dhidi ya Lucas Mbwiga Mwapenza kuhusiana na mgogoro wa Kitalu cha uchimbaji madini ya dhahabu eneo la Kisumain Kijiji cha Ifumbo Kata ya Ifumbo Wilaya ya Chunya yamepokelewa na Hakimu James Mhanusi kwa ajili ya kusikilizwa.
Hati hiyo imewasilishwa Mahakama ya Wilaya na Wakili wa kujitegemea Jacqueline Massawe kwa niaba ya Aidan Msigwa wakati Lucas Mwampenza akitetewa na Wakili Boniphace Mwabukusi akisaidiwa na Wakili Irene Mwakyusa.
Mashauri yaliyowasilishwa Mahakamani na Wakili Jacqueline Massawe kwa niaba ya Aidan Msigwa ni pamoja na kesi ya msingi ya kutaka kulimiliki eneo lake analodai kulimiliki kihalali baada ya kulinunua,shauri la pili ni kusudio la zuio la kutofanyika kwa shughuli zozote katika eneo hilo na shauri la tatu ni kuendelea na shughuli licha ya kuwepo kwa zuio la Mahakama.
Wakili Massawe amempatia Wakili Mwabukusi Hati ya dharula na nakala kuwasilishwa Mahakamani na Wakili Mwabukusi naye kuwasilisha pingamizi mbele ya Mahakama.
Baada ya kupokea nyaraka za pande zote mbili Hakimu James Mhanusi ameahirisha shauri hilo hadi mei 13,2024 Mahakama itakapoanza kuzisikiliza pande zote mbili.
Nje ya Mahakama Wakili Mwabukusi ameeleza mashauri anayodaiwa katika Mahakama hiyo kupitia Hati ya dharura kuwa ni pamoja na kesi ya msingi ya kutaka kulimiliki eneo lake analodai kulimiliki kihalali baada ya kulinunua,shauri la pili ni kusudio la zuio la kutofanyika kwa shughuli zozote katika eneo hilo na shauri la tatu ni kuendelea na shughuli licha ya kuwepo kwa zuio la Mahakama.
Mahakama pekee ndiyo inatarajiwa kuumaliza mgogoro huo ili kuleta amani katika Kata ya Ifumbo.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuwa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar utafanyika tarehe 08 Juni, 2024. Taarifa kwa umma iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Bw. Kailima, R. K jijini Dodoma leo tarehe 02 Mei, 2024 imesema kwamba fomu za uteuzi kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo zitatolewa kuanzia tarehe 17 hadi 23 Mei, 2024. Taarifa hiyo imefafanua kuwa uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 23 Mei, 2024 na kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo zitafanyika kuanzia tarehe 24 Mei, 2024 hadi tarehe 07 Juni,…
Jopo la Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi 50 kutoka Hospitali za Rufaa na Kanda ya Kusini wanaounda Kambi Rasmi ya Madaktari Bingwa wa Daktari Samia wamepiga Kambi katika Hospitali ya Rufaa ya Sokoine na kutoa huduma za afya za kibingwa kuanzia Jumatatu, Mei 06, hadi Ijumaa Mei 10, 2024. Akitoa tathmini ya kambi hiyo wakati wa ufunguzi rasmi, Daktari Alexander Makalla, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine ameeleza kuwa Madaktari bingwa na bobezi hao wanatoka katika Hospitali mbalimbali zilizopo nchini ikiwemo hospitali za Rufaa ya Sokoine RRH, Ligula RRH, hospitali za rufaa za Mkoa wa…
Benki ya Maendeleo(TIB) imekabidhi Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya(MBEYAUWSA) hundi ya Mkopo kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya maji Jijini Mbeya na Mji Mdogo wa Mbalizi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika Jijini Mbeya ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa ambaye ameitaka Benki kuwekeza zaidi zaidi Mkoani Mbeya kutokana na fursa nyingi zilizopo pia akiishukuru kutoa mkopo kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya TIB Lilian Mbasi amesema Kanda ya Nyanda za Juu Benki imewekeza zaidi ya shilingi bilioni sitini na Mkoa wa Mbeya ukiwa ni moja ya Mikoa iliyonufaika na mikopo.
Naye Zewena Hemed Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miradi anaeleza lengo la mkutano huo kuwa ni kueleza fursa mbalimbali zinazopatikana Benki ya TIB.
Aidha Mjumbe wa Bodi kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya(MBEYAUWSA)Hilda Ngoye amesema mkopo walioupata watautumia kama ilivyokusudiwa.
Baadhi ya Wadau wa mkutano huo wamepata fursa ya kutoa neno akiwepo Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya CPA Chiwanga na Mfanya biashara Machemba.
Benki ya TIB imekuwa ikitoa mikopo yenye riba nafuu kwa wafanyabiashara,wakulima,viwanda na Taasisi za kifedha nchini.
Mgogoro umeibuka baina ya Lucas Mbwiga na Aidan Msigwa Wawekezaji wawili wa machimbo ya dhahabu katika Kijiji cha Ifumbo Kata ya Ifumbo Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya ambapo kila mmoja anadai kulimiliki kihalali eneo la Kisumain lililokuwa na leseni ya uchimbaji wa madini kwa jina la Daud Mwantavila ambalo linadaiwa kupangishwa kwa Lucas bila ridhaa ya familia huku Aidan Msigwa akidai kulinunua kisheria na kubadilisha umiliki wa leseni kutoka kwa Daud na kuja kwake tangu April 22,2024.
Mkuu wa Progamu za Urithi wa Dunia wa Tume ya Taifa ya UNESCO Eric Kajiru akiwasilisha mada katika Semina ya wadau Maeneo ya Hifadhi za Asili ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Urithi wa Dunia Afrika yaliyofanyika Kitaifa wilayani Kondoa mkoani Dodoma *Fursa hiyo ipo kwa sasa kabla ya vigezo havijabadilika Na Mwandishi Wetu Tume ya taifa ya UNESCO imewataka wadau ambao wanataka kuziingiza maeneo yao katika orodha urithi wa dunia kuanza mchakato kabla ya 2027 kwani huenda taratibu zikabadilika na kuwa ngumu zaidi. Akiwasilisha mada kwa wadau wa maeneo ya hifadhi za asili na utamaduni katika maadhimisho ya…