Author: Mbeya Yetu

Baada ya Sintofahamu kutanda kufuatia hoja aliyoiwasilisha Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mh:Fransis Mtega Bungeni juu ya wananchi kupigwa na Askari wa TANAPA hoja ambayo ilimfanya Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kuiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kufika eneo husika mara moja na kushughurikia tatizo hilo tayari Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera amefika na kuzungumza na wananchi juu ya tukio hilo la kusikitisha.

Baada ya kuwasikiliza wananchi RC Homera amelaani Vikali kitendo kilichofanywa na Askari hao na ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata ndani ya saa 24 na kuwatia Mbaroni Askari hao waliohusika na kuongeza kuwa Serikali haijawahi kutuma Askari kupiga au kunyanyasa Raia bali jukumu la Askari ni kulinda Raia na Mali zake.

Read More

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza Mawaziri wanaohusika na utatuzi wa migogoro ya mipaka ikiwemo sekta za Ardhi, mifugo na Maliasili kwenda wilayani Mbarali mkoani Mbeya kushughulikia mgogoro unaodaiwa kuibuka hivi karibuni.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Mbarali Francis Mtega kutoa hoja kulitaka bunge kujadili kwa dharula mgogoro kwa taarifa kuwa mmoja wa wafugaji mifugo yake inashikiliwa na amedhamiria kujinyonga na hadi alipowasilisha hoja hiyo alikuwa bado anadhibitiwa na wananchi wanzake asitimize azma hiyo kwa sababu ya mifugo yake kukamatwa na kushikiliwa.

Akitoa majibu ya serikali kufuatia hoja hiyo Waziri Mkuu amewataka Mawaziri wote wa kisekta kwenda kutatua mgogoro huo haraka na kuwasilisha taarifa kamili ofisini kwake kesho saa mbili usiku.

Read More