Author: Mbeya Yetu

Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameishukuru Serikali kwa kusikiliza kilio cha Wananchi wa Mbeya kwa hatua ya kuanza kuboresha miundombinu mbalimbali katika Jiji la Mbeya ikiwemo barabara ambazo zimekuwa kero kwa miaka mingi.Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 27 Julai, 2024 wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba ya miradi ya TACTIC ujenzi wa barabara, Kituo Kikuu cha Mabasi na Soko Kuu la Jiji hilo iliyofanyika katika Viwanja vya Aiport ya zamani ambapo Mgeni rasmi akiwa ni…

Read More

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 26 Julai, 2024 amemkabidhi nyumba ya kuishi Mzee Ambalile Mwala ambaye amekuwa akiishi katika mazingira magumu pamoja na familia yake katika Kata ya Ching’anda Mlimba Mkoani Morogoro. Nyumba hiyo imejengwa na taasisi ya Tulia Trust.

Pamoja na hayo, Dkt. Tulia ametoa msaada wa madaftari, kiti mwendo kwa wahitaji na malumalu kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata ya Ching’anda Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

Read More