Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- Viongozi 11 wa CHADEMA washikiliwa na Polisi Mkoa wa Songwe
- ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAHUNDI ZANZIBAR
- Jinsi ya Kufikisha Malalamiko Kuhusu Mradi wa REGROW na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
- Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi Akagua Hali ya Mawasiliano Kisiwani Kojani, Pemba
- Inauma sana: Mtoto wangu kaenda chuo kikukuu katumbukia katika umalaya na dawa za kulevya
- WALIOKUWA WANAENDA KUMZIKA NEEMA ALIYEFIA KARIAKOO WAPATA AJALI, MMOJA AJARIKI
- Mbunge Jimbo la Busokelo Mh Mwakibete Serikali ya chama cha Mapinduzi imeitendea haki mkoa wa Mbeya
- Mbunge wa Kyela Ally Jumbe Kinanasi Awakumbusha wana Mbeya
Browsing: Video Mpya
Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza, ameendelea na ziara yake kwa mara nyingine baada ya kumalizika kwa vikao vya bunge akikutana na wananchi katika vijiji na kata mbalimbali ili kusikiliza kero zinazowakabili kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi na kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Mbunge Njeza ameendelea na ziara yake katika vijiji kadhaa vya kata za Iyunga Mapinduzi na Igale.
Akiwa katika kata ya Iyunga Mapinduzi amesikiliza kero za wananchi ambao kwa nyakati tofauti wameshukuru kwa namna miradi inayoendelea kutekelezwa ikiwemo usambazaji huduma ya umeme vijijini, usambazaji huduma ya maji na uboreshaji miundombinu ya elimu licha ya baadhi ya changamoto kuendelea kuwakabili.
Wananchi hao wameeleza kukabiliwa na kadhia ya bei kubwa ya huduma za afya hasa huduma ya upasuaji kwa akina mama.
“Sisi hapa tunamuomba mama yetu ni mwanamke kama sisi tunasikia anamwaga hela kwa Simba na Yanga basi atupunguzie bei za upasuaji na sisi huku maana hata mimi napenda Simba na Yanga”, ameeleza mwananchi wa kata ya Iyunga Mapinduzi Mwile Mboko.
Naye Rashid Fungambili mkazi wa kijiji cha Shuwa katani humo ameomba Serikali kupeleka daktari katika kijiji chao ambacho kina zahanati na kata ina kituo cha afya tarajiwa.
Mbunge Oran Njeza wa Mbeya vijijini, amepokea kero hizo kwa ajili ya kuziwasilisha kwa wataalam kuzitafutia ufumbuzi mara moja ambapo kuhusu huduma za afya kwa ujumla amewashauri wananchi wake kujiunga na bima ya afya kwa wote ili kupata matibabu hata wasipokuwa na fedha.
Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya ikiwemo kujenga na kuboresha vituo vya afya kuwa vya kimkakati na kwenye kata hiyo amesema kituo cha afya cha kimkakati kitajengwa ili kuhudumia kata za Iyunga Mapinduzi, Isuto na Itawa.
Kero nyingine ni pamoja na barabara hasa kuelekea msimu wa mvua ambapo Mbunge huyo amewaondoa hofu wananchi kwa kumuinua afisa kutoka wakala wa barabara Tanzania TANROADS mkoa wa Mbeya ambaye amesema barabara ya Mbalizi Shigamba (Km 52) inaanza kujengwa Oktoba 2024.
Kuhusu barabara ya Iyunga Mapinduzi kwenda Shisonta afisa kutoka wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA Mhandisi Mollel ameipokea na kuahidi TARURA kuiingiza kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha (2025-2026) ili ijengwe kwa kiwango bora.
“Mheshimiwa Mbunge kuhusu barabara hii ya Iyunga Mapinduzi Shisonta naomba nichukue, tutaiingiza kwenye bajeti ya 2025-2026”, ameeleza Mhandisi Mollel.
Pamoja na hayo Mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Mhe. Oran Manasse Njeza, ameendelea kuhimiza wananchi kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao shuleni ambapo katika kila shule aliyopita amechangia shilingi laki mbili ili kuwaunga mkono wananchi hao.
Sharif Abdul Afisa Mwandamizi kitengo cha mahusiano Jamii na ujirani mwema hifadhi ya Taifa Ruaha amesema kupitia mradi wa REGROW wameandaa Muongozo rafiki wa kupokea na kushughulikia malalamiko kutoka kwa wananchi wanaozunguka hifadhi.
Amesema kupitia mradi wa REGROW viongozi na kamati za kushughulikia malalamiko kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka mkoa wamejengewa uwezo kwa kupewa elimu namna ya kutumia muongozo huo ili kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi. Lengo nikuhakikisha wananchi wanaoathirika na shughuli za hifadhi au Mradi wa REGROW wanawasilisha malalamiko yao na yanashughulikiwa kwa utaratibu unaofahamika.
Aidha Abdul amewasihi wananchi wenye malalamiko wafike ofisi za Serikali ya Kijiji nakuwasilisha malalamiko yao au wapige simu ya bure moja kwa moja kwa Hifadhi ya Taifa Ruaha namba 0800110801 na Wizara ya Maliasili na Utalii namba 0800110804 endapo lalamiko linahusu Hifadhi au Mradi wa REGROW. Malalamiko yote yatashughulikiwa kwa usiri na mlalamikaji atalindwa na sheria na tararibu za nchi.
Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amehitimisha ziara yake ya siku tatu kutembelea watoa huduma za mawasiliano zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam.
Amehitimisha ziara yake kwa kutembelea Kampuni ya TIGO ambapo amefurahishwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Kampuni hiyo sanjari na kutoa ajira kwa zaidi ya vijana mia tano.
Amesema uwekezaji uliofanywa unaendana na kasi ya dunia zaidi wakiungana na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha huduma za mawasilano zinatolewa kwa ufanisi mkubwa.
Ziara yake Jijini Dar es Salaam imehusisha Kampuni ya Airtel, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kuhitimisha Kampuni ya TIGO