Browsing: Video Mpya

Mashauri matatu yalizofunguliwa Mahakama ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya kwa Hati ya dharula na Aidan Msigwa dhidi ya Lucas Mbwiga Mwapenza kuhusiana na mgogoro wa Kitalu cha uchimbaji madini ya dhahabu eneo la Kisumain Kijiji cha Ifumbo Kata ya Ifumbo Wilaya ya Chunya yamepokelewa na Hakimu James Mhanusi kwa ajili ya kusikilizwa.

Hati hiyo imewasilishwa Mahakama ya Wilaya na Wakili wa kujitegemea Jacqueline Massawe kwa niaba ya Aidan Msigwa wakati Lucas Mwampenza akitetewa na Wakili Boniphace Mwabukusi akisaidiwa na Wakili Irene Mwakyusa.

Mashauri yaliyowasilishwa Mahakamani na Wakili Jacqueline Massawe kwa niaba ya Aidan Msigwa ni pamoja na kesi ya msingi ya kutaka kulimiliki eneo lake analodai kulimiliki kihalali baada ya kulinunua,shauri la pili ni kusudio la zuio la kutofanyika kwa shughuli zozote katika eneo hilo na shauri la tatu ni kuendelea na shughuli licha ya kuwepo kwa zuio la Mahakama.

Wakili Massawe amempatia Wakili Mwabukusi Hati ya dharula na nakala kuwasilishwa Mahakamani na Wakili Mwabukusi naye kuwasilisha pingamizi mbele ya Mahakama.

Baada ya kupokea nyaraka za pande zote mbili Hakimu James Mhanusi ameahirisha shauri hilo hadi mei 13,2024 Mahakama itakapoanza kuzisikiliza pande zote mbili.

Nje ya Mahakama Wakili Mwabukusi ameeleza mashauri anayodaiwa katika Mahakama hiyo kupitia Hati ya dharura kuwa ni pamoja na kesi ya msingi ya kutaka kulimiliki eneo lake analodai kulimiliki kihalali baada ya kulinunua,shauri la pili ni kusudio la zuio la kutofanyika kwa shughuli zozote katika eneo hilo na shauri la tatu ni kuendelea na shughuli licha ya kuwepo kwa zuio la Mahakama.
Mahakama pekee ndiyo inatarajiwa kuumaliza mgogoro huo ili kuleta amani katika Kata ya Ifumbo.

Benki ya Maendeleo(TIB) imekabidhi Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya(MBEYAUWSA) hundi ya Mkopo kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya maji Jijini Mbeya na Mji Mdogo wa Mbalizi.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika Jijini Mbeya ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa ambaye ameitaka Benki kuwekeza zaidi zaidi Mkoani Mbeya kutokana na fursa nyingi zilizopo pia akiishukuru kutoa mkopo kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya TIB Lilian Mbasi amesema Kanda ya Nyanda za Juu Benki imewekeza zaidi ya shilingi bilioni sitini na Mkoa wa Mbeya ukiwa ni moja ya Mikoa iliyonufaika na mikopo.

Naye Zewena Hemed Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miradi anaeleza lengo la mkutano huo kuwa ni kueleza fursa mbalimbali zinazopatikana Benki ya TIB.

Aidha Mjumbe wa Bodi kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya(MBEYAUWSA)Hilda Ngoye amesema mkopo walioupata watautumia kama ilivyokusudiwa.

Baadhi ya Wadau wa mkutano huo wamepata fursa ya kutoa neno akiwepo Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya CPA Chiwanga na Mfanya biashara Machemba.

Benki ya TIB imekuwa ikitoa mikopo yenye riba nafuu kwa wafanyabiashara,wakulima,viwanda na Taasisi za kifedha nchini.