Browsing: Video Mpya

Mgogoro umeibuka baina ya Lucas Mbwiga na Aidan Msigwa Wawekezaji wawili wa machimbo ya dhahabu katika Kijiji cha Ifumbo Kata ya Ifumbo Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya ambapo kila mmoja anadai kulimiliki kihalali eneo la Kisumain lililokuwa na leseni ya uchimbaji wa madini kwa jina la Daud Mwantavila ambalo linadaiwa kupangishwa kwa Lucas bila ridhaa ya familia huku Aidan Msigwa akidai kulinunua kisheria na kubadilisha umiliki wa leseni kutoka kwa Daud na kuja kwake tangu April 22,2024.

20 WAFIKISHWA MAHAKAMANI 6 WAHOJIWA KWA KUTENGENEZA MFUMO BANDIA(POSS)WA KUKUSANYIA MAPATO MBEYA

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Mkoa wa Mbeya imewakamata na kuwafikisha mahakamani watu ishirini kwa kutengeneza mfumo bandia wa kukusanyia mapato kwa njia ya mtandao(Poss) na kutakatisha fedha na wengine sita wakiendelea kuhojiwa na TAKUKURU Mkoa wa Mbeya na ikithibitika watafikishwa mahakamani ambapo kwa pamoja wanadaiwa kuisababishia hasara Serikali zaidi ya shilingi bilioni moja.

Akitoa taarifa kwa wanahabari Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya Maghela Ndimbo amesema taarifa iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali imeeleza kuwepo na udukuzi wa fedha na kutengeneza mfumo bandia wa ukusanyaji ushuru wa mazao kutoka Halmashauri za Makete, Mbarali, Tunduma,Ileje,Rungwe,Busokelo,Jiji la Mbeya, Mbeya,Pangani na Manispaa ya Sumbawanga mfumo ambao hausomani na mtandao wa Serikali.

Uchunguzi wa awali uliwakamata watu thelathini na moja wakiwemo Wataalamu wa TEHAMA kutoka Halmashauri ambapo ishirini wamefikishwa mahakamani kwa kuisababishia hasara Serikali na kumi na moja kuachiwa huru.

Maghela Ndimbo amesema watu hao wamesababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni mia tatu.

Maghela amewataja watuhumiwa kuwa ni pamoja na Robert Mpeleta,Anold Nzali,Isaya Andembwisye,Mbwigane Mawamelo,Peter Joseph, Benedict Milinga,Hyeli Mkwama,Harid Habib,Fadhili Fredy,Lwesya Shukuru, Daniel Tweve,Ezekia Adam,Paul Samson na Ulimboka Adamson.

Watuhumiwa sita walifunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi katika Wilaya ya Mbarali kesi namba 24/2023 Asante Mwilapa, Stanford Bukuku na Afrika Mwambogo kwa pamoja wanadaiwa kuisababishia hasara ya shilingi laki mbili na elfu tisini na sita ambapo kesi ya uhujumu uchumi namba 25/2023 ambapo Ndundu Hitla anadaiwa kuisababishia hasara Serikali shilingi laki sita na elfu thelathini na sita pia kesi namba 26/2023 watuhumiwa wawili Elieck Luwale na Luwi Godigodi ambao wanatuhumiwa kuisababishia hasara Serikali shilingi laki moja hamsini na nne elfu na nne.

Aidha Ndimbo amesema watuhumiwa katika kesi namba 24/2023 na 26/2023 wapo nje kwa dhamana isipokuwa mshitakiwa kesi namba 20/2023 yupo mahabusu baada ya kukiuka masharti ya dhamana na washitakiwa wengine katika kesi ya uhujumu uchumi namba 03/2023 wamekosa dhamana kwa kuwa makosa ya utakatishaji fedha hayana dhamana.

Katika hatua nyingine TAKUKURU Mkoa wa Mbeya kwa kishirikiana na Afisa Mtendaji wa Kata ya ya Chimala Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali imefanikiwa kurejesha nyumba ya mjane aitwaye Bi Emelda Omary Pangani mkazi wa Chimala ambaye nyumba yake ilitwaliwa kwa nguvu na Baraka Ally Mboya baada ya mtoto wa mjane aitwaye Tamimu Halifa Mwenda kukopa kwa Baraka shilingi milioni sita na kuiba hati ya nyumba na kuikabidhi kwa Baraka ambapo Mahakama ya Mwanzo Chimala ilimhukumu kifungo cha miezi sita na kuamriwa kurejesha fedha kwa Baraka.

Pia katika hatua nyingine TAKUKURU Mkoa wa Mbeya imefuatilia miradi ya maendeleo ishirini na sita yenye thamani ya shilingi 149,728,128,096.32 ya sekta za Elimu,umwagiliaji, Maji na Mifugo.

#mbeyayetutv
Diwani wa kata ya Itezi Sambwee Shitambala amewaita waathirika wa maporomoko ya mlima Kawetere yaliyoathiri kaya 21 za Kata ya Itezi ambao waliweka kambi katika shule ya msingi ya Tambukareli na kuhudhuriwa na viongozi wa CCM na CHADEMA.

Katika kikao hicho viongozi wa CCM na CHADEMA walitupiana makombora wakidai uongozi uliopita chini ya CHADEMA ndio ulioruhusu kugawa viwanja katika maeneo hatarishi.