Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- Jinsi ya Kufikisha Malalamiko Kuhusu Mradi wa REGROW na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
- Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi Akagua Hali ya Mawasiliano Kisiwani Kojani, Pemba
- Inauma sana: Mtoto wangu kaenda chuo kikukuu katumbukia katika umalaya na dawa za kulevya
- WALIOKUWA WANAENDA KUMZIKA NEEMA ALIYEFIA KARIAKOO WAPATA AJALI, MMOJA AJARIKI
- Mbunge Jimbo la Busokelo Mh Mwakibete Serikali ya chama cha Mapinduzi imeitendea haki mkoa wa Mbeya
- Mbunge wa Kyela Ally Jumbe Kinanasi Awakumbusha wana Mbeya
- Mhe. Bahati Ndingo. Uvungu kwa uvungu kitanda kwa kitanda ili Mbarali iendelee kuwa chini ya CCM
- MH. MASACHE. SIKU SABA ZA MOTO CHUNYA TUMEITIKA
Browsing: Video Mpya
Maji ya ziwa Rukwa ni rasilimali muhimu kwa maisha ya wananchi wa mikoa kadhaa ya Nyanda za Juu Kusini kwa ajili ya matumiziya binadamu na uzalishaji wa mali
katika makala haya tunangazia juhudi zinazochukuliwa na mko wa Katavi ktika kulinda ikolojia ya ziwa hilo.
Kijungu na Daraja la Mungu ni maeneo maarufu ya kijiografia na vivutio vya utalii nchini Tanzania, vilivyopo katika mkoa wa Mbeya, Nyanda za Juu Kusini. Zina sifa za asili za kijiolojia zinazovutia watalii na watafiti wa mazingira.
Kijungu
Kijungu ni eneo la kijiolojia lenye sura ya mto unaozunguka mwamba mkubwa, na kuacha mduara kama “jungu” (sufuria), na ndilo linalotoa jina lake. Hapa maji ya mto huchonga mwamba kwa nguvu, na kuacha mandhari ya kuvutia. Kijungu kinajulikana kwa nguvu zake za maji ya maporomoko ambayo yamepita hapo kwa miaka mingi, na kuunda maumbo haya ya kustaajabisha.
Daraja la Mungu
Daraja la Mungu ni jiwe kubwa lililojitengeneza kiasili na kuonekana kama daraja la asili. Inasemekana kuwa ni sehemu ya maporomoko ya maji ambayo maji yamechonga miamba kwa muda mrefu, na kuacha mwamba huo mkubwa ukionekana kama daraja. Jina “Daraja la Mungu” limetokana na imani za wenyeji kuwa daraja hilo limeundwa kwa nguvu za kimuujiza, kutokana na umbo lake la kipekee.
Maeneo haya yote ni sehemu muhimu za utalii wa mazingira nchini Tanzania, na huvutia watu wanaopenda urembo wa asili, kijiolojia, na historia ya asili ya Tanzania.
Samadi ya ng’ombe imekuwa ikuchukuliwa kama uchafu unaochangia uharibifu wa mazingira mitaani, lakini kwa wananchi wa Wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwao hali ni tofauti kwani sasa wanaityumia samadi hiyo kuokoa uhribifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa. Makala haya yanaelezea namna wananchi hao wanavyotumia samadi hiyo kutengeneza gesi ya kupikia (Biogas),.
Tabia ya baadhi ya Wazazi kuwapiga watoto wao kupita kiasi bila kujali athari za kiafya na kisaikolojia zitakazompata mtoto husika ni aina ya ukatili kwa watoto.. Makala hii inaeleza madhara yaliyompoata mtoto mmoja wa kike wilyani Mbozi mkoani Songwe baada ya kupigwa na Baba yake mzazi kwa tuhuma za kuiba pesa nyumbabni.kwao. Kupitia mradi wa Ulinzi na Usalama wa mtoto Shirika la Intergrated Rule Development Organisation limeingilia kati ukatili huoili kumuokoa mtoto huyo dhidi ya ukatili aliofanyiwa.
Na. Mwandishi Jeshi la Polisi Arusha.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limezindua kampeni ya tuwaambie kabla hawajaharibiwa kwa lengo la kuongea na wanafunzi kuanzia elimu ya awali hadi vyuo vikuu kwa ajili ya kuwaelimisha juu ya kujitambua ili kujiepusha na vitendo vya mmomonyoko wa maadili.
Akizungumza katika uzinduzi huo ambao umehudhuriwa na washiriki zaidi ya 3,000, Katibu Tawala Msaidizi viwanda Biashara na uwekezaji Mkoa wa Arusha Bw. Frank Mbando ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amewataka wanafunzi kuhakikisha wanajitunza vyema na kuwa makini na rika walilopo kwa kujiepusha na vitendo ambavyo vitaharibu maisha yao ya sasa na ya baadaye.
Aidha amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika elimu kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bure yenye ubora ambapo amesema hadi sasa zaidi ya shilingi bilioni saba zimeshatolewa tangu serikali ya awamu ya sita iingie madarakani.
Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi SP Happiness Temu amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwatahadharisha wanafunzi wa shule za awali Msingi, Sekondari na vyuo vya juu kuacha kuiga tabia mbovu ambazo hazina tija katika ustawi wa Maisha yao ya kila siku na masomo.
SP Temu amebainisha kuwa kupitia elimu ambayo itaenda kutolewa itasaidia kujenga taifa litakalokuwa na kizazi chenye maadili mema na raia wema wanaojitambua kabla ya kupitia mapito ya ukatili.
Kamanda wa Kikosi Cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua amesema dhima ya Jeshi la Polisi kupitia kampeni hiyo ni kuhakikisha linayafikia makundi yote ya wanafunzi kuanzia shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vya ngazi zote kuzungumza nao kuwapa elimu ya kujitambua mapema.
Katika uzinduzi wa Kampeni hiyo Washiriki zaidi ya 3,000 ambao ni Jeshi la Polisi, Shule zaidi ya 10, vyuo 12 pamoja na Wananchi walishiriki.