Browsing: Video Mpya

#mbeyayetutv

SIMBA WAVAMIA VIJIJI WATAFUNA MIFUGO TANANGOZI IRINGA
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa ameambatana na wajumbe wa kamati hiyo na kuwatoa hofu wananchi wa kijiji cha tanangozi kutokana na taharuki ya simba wanaodaiwa kula mifugo yao na kutishia usalama wa maisha yao.

RC Dendego amesema jambo hilo linafanyiwa kazi na zoezi la kuwatafuta simba hao linaendelea hivyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya wanyama hao.

“Naomba wananchi mshiriki kutoa taarifa tu na kazi ya kuwatafuta na kuwakamata waachieni wataalamu wa wanyamapori”amesema RC Dendego

Kwa upande wake Mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha Godwell Ole Meing’ataki amewataka wananchi kuwa watulivu kwani wamejipanga kuhakikisha wanawapata simba hao haraka iwezekanavyo kabla awajaleta madahara Kwa binadamu.

Pi amewatahadharisha wananchi kuto kula mabaki ya mifugo hiyo Kwa kuwa kwenye zoezi la kuwakamata Simba hao wanatumia mbinu mbalimbali ikiwemo kutumia madawa ya usingizi kwa kuweka kwenye masalia ya mifugo hiyo Kwa sababu Simba ana tabia ya kula na kubakiza mzoga na Kisha anarudia tena.

TAARIFA YA AFISA HABARI OFISI YA MKUU WA MKOA WA IRINGA.