Author: admin

Baadhi ya Watumishi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wakisherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakipita mbele ya jukwaa kuu. Baadhi ya Watumishi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wakiwa katika maandamano ya Kuingia katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha ambapo Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yanafanyika Kitaifa. Baadhi ya Watumishi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wakiwa katika Picha ya Pamoja wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kitaifa yanafanyika jijini Arusha. Baadhi ya Watumishi wa Tume Huru ya…

Read More

JESHI LA POLISI LAPONGEZWA KWA UPENDO WAO KWA WANANCHI.

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi- Dar es salaam

Mkuu wa Gereza Kuu Ukonga Kamishina msaidizi wa Magereza ACP Dkt. Juma Mwaibako amelipongeza Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo linashirikisha jamii katika kubaini,kutanzua na kuzuia uhalifu hapa nchini.

Hayo ameyasema wakati anapokea misaada mbalimbali kutoka kwa askari Polisi waliotimiza miaka nane ya utumishi ndani ya Jeshi hilo ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo limebadilika sana kiutendaji ambao unaoendana na mabadiliko ya dunia.

Kwa upande wake mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msaidizi wa Polisi Amosi Mikao amesema wametoa misaada hiyo ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa Mwezi Mungu kwa kuwalinda katika kazi zao.

Nae Rosemary Mitula mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msaidizi wa Polisi amesema waliona waungane kulikumbuka kundi hilo ambalo lina mchango pia katika jamii na taifa kwa ujumla kiuchumi kwa kuwasadia vifaa mbalimbali katika gereza kuu la Ukonga lilipo jijini Dar es salaam.

Read More