Browsing: Video Mpya

MADEREVA WANAOTUMIA LUGHA CHECHEFU KWA ABIRIA WAONYWA.
Na. Abel Paul, Jeshi la Polisi Arusha.
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini limewataka madereva kufuata sheria za Usalama Barabarani ambapo limewataka madereva hao kutoa lugha nzuri na rafiki kwa abiria Pamoja na kuongea nao kabla ya safari kuanza huku likiwapiga faini madereva ambao hawana sanduku la dhalula.
Akiongea leo Alfajiri octoba 16,2024 Katika kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani na Nchi Jirani jijini Arusha Mkuu wa kitengo cha Elimu kwa Umma na Mafunzo kutoka Makao Makuu ya kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Michael Deleli amewaonya na kuwataka madereva kutumia lugha nzuri kwa abiria wanaowahudumia.
Ameongeza kuwa endapo dereva hatopata shukrani kutoka kwa abiria atambue kuwa ajatoa huduma nzuri kwa abaria wake ambapo amewataka madereva kufuata sheria za usalama barabarani na kutoa huduma nzuri ili abiria waridhike na huduma wanazotoa kila mara.
ACP Deleli akasisitiza suala la kuongea na abiria kabla ya safari ili kutambua changamoto za abiria wao huku akiwataka kutumia lugha nzuri amabazo wanazitoa kwa wateja wao kabla na wakati wote wa safari.
Nae Domisiano Msakalile ambaye ni miongoni mwa abiria wanatumia vyombo hivyo licha ya kushukuru kikosi cha usalama barabarani nchini kwa kuendelea kutoa elimu kwa madereva na abiria amebainisha kuwa elimu hiyo imemuongezea maarifa na utambuzi wa mambo na haki zake kama abiria anayetumia vyombo hivyo.
Kwa upande wa madereva wanaofanya safari zao kutoka Mkoani Arusha Kwenda mikoa mbalimbali na nchi Jirani pamoja na kushukuru kikosi cha usalama Barabarani kwa kutoa elimu wakawaangushia lawama abiria ambao wamekuwa wakiwalazimisha kushuka na kupata huduma mbalimbali za kijamii maeneo yasio ruhusiwa kupata huduma husika.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) leo tarehe 14 Oktoba, 2024 amejiandikisha kwenye Daftari la Mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Akizungumza na wananchi wa mtaa wa Mayombol uliopo Kata ya Iwambi, mkoani Mbeya Naibu Waziri Mahundi ametoa wito kwa wananchi hao kujitokeza na kushiriki katika zoezi la kujiandikisha ili waweze kumchagua kiongozi bora atakayewezesha shughuli mbalimbali za maendeleo ya maeneo yao.

MRADI WA REGROW KUCHOCHEA UCHUMI WA WANANCHI WANAOPAKANA NA HIFADHI KUSINI MWA TANZANIA
Wananchi wa vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Ruaha, Mikumi, Udzungwa na Nyererevinanufaika na Mradi wa REGROW unaotekelezwa nchinikupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia.
Hayo yamesemwa Jijini Mbeya na Bi. Blanka Aquilinus Tengia Naibu Msimamizi wa Mradi wa REGROW unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na kutekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na TANAPA, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) na Bodi ya Bonge la Maji Rufiji (RBWB).Lengo la mradi ni kuboresha usimamizi wa maliasili sanjari na kukuza utalii Kusini mwa Tanzania.
Blanka Tengia amesema mradi ulianza mwaka 2017 baada ya tafiti mbalimbali kufanyika na ni wa thamani ya Dola za marekani milioni 150 sawa na takribani shilingi za kitanzania bilioni 345.
Aidha, moja ya shughuli zinazotekelezwa ni kuboresha miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege na majengo ndani ya hifadhi nne za kipaumbele. na miundombinu ya maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Mbali ya kuboresha miundombinu Mradi wa REGROW unachochea ukuaji wa wa wananchi kiuchumi hususani wanaoishi nyirani na hifadhi zilizotajwakwa kusaidia uanzishwaji wa miradimiradi mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi, ufadhili wa masomo kwa vijana, vikundi kupewa mtaji wa kukopeshana kwa riba nafuu na kuiwezesha jamii kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu. Pia mradi unatekeleza shughuli za utunzaji wa vyanzo vya maji kwenye eneo la juu la Hifadhi ya Taifa Ruaha ambavyo ni vyanzo vya maji kwa mto Ruaha Mkuu.
Katika hatua nyingine Blanka amesihi wananchi wanaoishi pembezeno mwa hifadhi kuzipenda na kuzitunza hifadhi hizo na kufanya Utalii wa ndani ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kukuza Utalii kupitia filamu ya The Royal Tour.