Afisa anayeshughulikia malamiko Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Francis Mhina amesema taasisi yake imerahisisha upatikanaji wa ujenzi wa vituo vya mafuta maeneo ya mijini na vijijini.
Ameyasema hayo katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Nyanda za Juu yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya.
Katika hatua nyingine Mhina amesema mwananchi mwenye malalamiko juu ya utendaji usioridhisha kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira,Shirika la Umeme na Vituo vya mafuta ofisi yake ipo wazi kupokea chamoto hizo.
Tobieta Makafu Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambayo inahudumia Mikoa ya Mbeya,Njombe,Songwe na Rukwa amesema endapo mwananchi atauziwa mafuta kinyume na bei elekezi asisite kutoa taarifa EWURA.