Kituo cha Radio Highlands Fm 92.5 Mbeya kwa kushirikiana na Kampuni ya 3 Ocean imezindua mchezo wa kubahatisha nchini unaofahamika kwa jina la Vuna Deile ambapo Washindi watajinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo gari,pikipiki,TV na pesa taslimu.
Akitoa taarifa kwa Wanahabari Mkurugenzi wa Kituo cha Radio Highlands Fm Mbeya Jacqueline Mwakyambiki amesema mchezo huu wa Vuna Deile ni rahisi utachezwa na mtu yeyote kwa njia ya simu yake ya mkononi ambako Radio inasikika nchini na unachezwa kuanzia kiasi cha shilingi mia mbili tu.
Jacqueline amewataka wananchi kuichangamkia fursa hii hususani wale wa Mikoa ya Mbeya,Songwe na Njombe kwani ni wa kusisimua ambao pia utawaongezea kipato kwa muda mfupi tu.
Naye Ron Fidanza Afisa masoko wa Kampuni ya 3 Ocean amesema mbali ya washindi kupata zawadi mchezo huu utatoa ajira kwa vijana mbalimbali Mkoani Mbeya hivyo wananchi wanapaswa kuchangamkia fursa hii adhimu.
Fidanza amesema mchezo huu utatoa mshindi kila siku kupitia simu yake ya mkononi kwa kupiga *150*80# itakuja namba 2 utachagua kiwango cha kucheza kuanzia shilingi mia mbili na kuendelea.
Tabu Hamis Mwanakatwe mkazi wa Soweto Kata ya Ruanda Jijini Mbeya ni mmoja wa washindi waliojinyakulia zawadi amesema mchezo huo ni rahisi kucheza ambapo alicheza kwa shingi mia mbili na kujinyakulia shilingi elfu ishirini na matarajio yake ni kucheza mara kwa mara ili ajinyakulie zawadi mbalimbali.
Aidha Situmai Abdallah mkazi wa Isyesye Jijini Mbeya amesema yeye alicheza kwa shilingi mia mbili na kujinyakulia shilingi elfu ishirini na kupia fedha hiyo imemuongezea mtaji kwenye biashara yake.
Baadhi ya zawadi zimeoneshwa hadharani ambapo zimehanikizwa na matangazo mbalimbali yaliyoambatana na maandamano ya bodaboda kauli mbiu ya mchezo ni “Panda,Vuna,Timiza ndoto”.