Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) Kanda ya Nyanda za Juu ni miongoni mwa Taasisi za Umma zinazoshiriki maonesho ya Biashara ya Mbeya City Expro 2024 yanayoendelea katika Soko la Zamani la Uhindini Jijini Mbeya yaliyoanza mei 22,2024 na yatatamatika mei 30,2024.
Mmoja wa washiriki mkazi wa VETA Jijini Mbeya Agrey Kiwale aliyetembelea Banda la NEMC amefurahishwa na elimu aliyoipata kupitia maonesho hayo hivyo ametoa wito kwa wananchi kutembelea maonesho hayo ili kujifunza utunzaji wa mazingira.
Kupitia maonesho hayo wananchi pamoja na Taasisi mbalimbali zinakaribishwa kutembelea Banda la NEMC ili kujifunza shughuli zinazotekelezwa zikiwemo za upandaji miti na utunzaji wa mazingira.