Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imeendelea kung’ara na kuvunja rekodi kwa kutoa wafanyakazi hodari kwa vipindi viwili (mwaka 2022 na 2024).
Hatua hii imefikiwa baada ya mfanyakazi hodari Joshua J. Kusaga, Fundi Sanifu vifaa tiba, kuchaguliwa kuwa mfanyakazi hodari Mei Mosi kitaifa.
Katika hafla iliyofanyika jijini Arusha, Joshua alikabidhiwa zawadi na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya inajivunia kuwa na wafanyakazi wenye uwezo mkubwa na inaendelea kuweka msisitizo katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi. Mfanyakazi huyu ameonyesha uwezo, bidii na utaalamu wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yake.
Tunampongeza Joshua J. Kusaga kwa mafanikio haya makubwa na tunamtia moyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uaminifu ili kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya nchini.
Trending
- DKT TULIA ACKSON ASHIRIKI IBADA BAPTIST ISYESYE MADHABAHU YA REHEMA NA SAUTI YA UPONYAJI
- CHADEMA CHUNYA YALIA NA UKOSEFU WA MAGARI POLISI, WAGOMBEA WAFUNGUA KAMPENI
- KUMEKUCHA KAMPENI ZA CCM MBEYA VIJIJINI, MBUNGE NJEZA ASEMA DKT SAMIA KASAFISHA NJIA
- EZEKIA ZAMBI MWENYEKIT ACT WAZALENDO
- CHADEMA LUPA YATUMA SALAMU ZA KUIONDOA CCM IKIZINDUA KAMPENI, KERO ZAAINISHWA
- Huyu mwanamke anadai mimba yangu haionekani tumboni kwake!
- Fedha zangu zote za kustaafu zilikuwa zinateketea hadi nilipoamua kufanya hivi
- POLISI NA WANAHABARI MBEYA WAWEKA MIPANGO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA