Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imeendelea kung’ara na kuvunja rekodi kwa kutoa wafanyakazi hodari kwa vipindi viwili (mwaka 2022 na 2024).
Hatua hii imefikiwa baada ya mfanyakazi hodari Joshua J. Kusaga, Fundi Sanifu vifaa tiba, kuchaguliwa kuwa mfanyakazi hodari Mei Mosi kitaifa.
Katika hafla iliyofanyika jijini Arusha, Joshua alikabidhiwa zawadi na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya inajivunia kuwa na wafanyakazi wenye uwezo mkubwa na inaendelea kuweka msisitizo katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi. Mfanyakazi huyu ameonyesha uwezo, bidii na utaalamu wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu yake.
Tunampongeza Joshua J. Kusaga kwa mafanikio haya makubwa na tunamtia moyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uaminifu ili kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya nchini.
Trending
- MAHUNDI AZINDUA VIKOBA DAR ES SALAAM
- MHESHIMIWA MHANDISI MARYPRISCA MAHUNDI AZINDUA KIKUNDI CHA VICOBA DAR ES SALAAM
- Jinsi mume alivyomuokoa mkewe kufanyiwa upasuaji kipindi akijifungua
- SHUHUDIA VIPAJI VYA WANAFUNZI WANAOTARAJIA KUANZA DARASA LA KWANZA 2025 MARYS PRE &PRIMARY SCHOOL
- Hii ndio sababu elimu pekee haiwezi kukusaidia kupata ajira
- CHAUMMA YAGAWA UBWABWA KUSHEREKEA USHINDI WA UENYEKITI WA MTAA
- Nilivyomrejesha mume tuliyeachana kwa talaka
- Viongozi wa Dini Wapongeza Utulivu na Amani Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa