Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonaz akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kilichokutana Mjini Unguja Zanzibar leo Juni 9,2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonaz (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Tume, Ramadhani Kailima, wakati Katibu Mkuu huyo alipofika kufungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Tume Mjini Unguja, Zanzibar leo Juni 9,2025.
Na. Mwandishi Wetu, Zanzibar
na Uratibu), Dkt. Jim Yonaz ameipongeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa
kukamilisha zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na
kuendelea vyema na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Dkt. Yonazi ametoa pongezi hizo leo tarehe 09
Juni, 2025 Kisiwani Unguja, Zanzibar wakati wa kufungua kikao cha Baraza la
Wafanyakazi la INEC, ambapo imewaasa
viongozi wa Tume kuendelea kuwa imara na kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano
ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unakwenda vizuri.
“Kwanza niwapongeze sana kwa kukutekeleza
jukumu hili kubwa ambalo mmekabidhiwa na Taifa letu na kwa namna ya pekee
kabisa Mwenyekiti wa Baraza unifikishie salamu za pongezi kwa Mwenyekiti wa
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele pamoja na
wajumbe wa Tume kwa kazi kubwa ambayo mmeifanya katika kuhakikisha kuwa
shughuli za uchaguzi nchini kwetu zinakwenda vizuri,” amesema Dkt. Yonazi.
Ameeleza kuridhishwa na jinsi Tume ilivyotekeleza
kwa ufanisi zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuongeza
kuwa ni matarajio ya Serikali kuwa utendaji huo mzuri wa Tume utaendelea kwa
viwango vya juu kwa mujibu wa katiba, sheria na taratibu mbalimbali ambazo zimewekwa.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti
wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya
Taifa ya Uchaguzi, Ndugu. Kailima Ramadhan amesema tayari Tume imekamilisha
awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo kwa
sasa inaendelea na uboreshaji wa awamu ya pili.
“Tume imeshakamilisha uboreshaji wa awamu ya
kwanza na imeshachakata na kutoa daftari la awali na imeshakamilisha uboreshaji
wa awamu ya pili mzunguko wa kwanza na mzunguko wa pili. Tunategemea kuanzia
tarehe 28 mwezi huu (tarehe 28 Juni, 2025) tutaanza mzunguko wa tatu wa
uboreshaji katika Vyuo vya Mafunzo Tanzania Zanzibar na Magereza Tanzania Bara
kwa wanafunzi na wafungwa waliohukumiwa kifungo chini ya miezi sita,” amesema
Kailima.
Katibu huyo wa Baraza amesema mzunguko huo wa
tatu utahusisha vituo 140 vya kuandikisha wapiga kura ambapo 130 vipo kwenye
magereza Tanzania Bara na vituo 10 vipo kwenye vyuo vya mafunzo Tanzania
Zanzibar. Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku saba hadi tarehe 04 Julai,
2025.
Ameongeza kuwa Tume imekamilisha maandalizi
ya nyaraka mbalimbli kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni pamoja
na Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025, Kanuni za
Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025 na maelekezo
mbalimbali kwa ajili ya watendaji wa uchaguzi na wadau wa uchaguzi kupata
miongozo kwa ajili ya utekelezaji wa uchaguzi.
Alimkumbusha mgeni rasmi kuwa tayari Tume
imekamilisha zoezi la ugawaji wa majimbo na kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa
mwaka 2025 kutakuwa na jumla ya majimbo 272 yatakayofanya uchaguzi wa wabunge
katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kata 3960 kwa ajili ya uchaguzi wa
madiwani kwa Tanzania Bara.