Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Ndele Mwaselela, amekutana na waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi kuhusu uvumi unaoenea miongoni mwa baadhi ya wanachama wa chama hicho kuwa amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini.
Katika tamko lake kwa vyombo vya habari, Mwaselela amekanusha taarifa hizo na kusisitiza kuwa hana nia ya kugombea ubunge bali anaendelea kujikita kikamilifu katika kulitumikia Chama katika nafasi yake ya uongozi ndani ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.