Rais wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu Ndoto ya Yatima kilichoandikwa na Shukurani Gideon Mwasanjobe, Mkurugenzi wa Tehla Foundation (TEFO) na mmiliki wa Shule ya Sekondari Vanessa. Uzinduzi huo utafanyika Septemba 13, 2025 jijini Mbeya.
Kwa kaulimbiu “Tambua Thamani ya Ndoto Iliyojificha Ndani ya Yatima”, kitabu hiki kinalenga kuibua ari na matumaini kwa watoto yatima. Mratibu wa tukio, George Mwaitenda, amesema uzinduzi huo utahusisha ushuhuda kutoka kwa watoto waliowahi kunufaika na malezi ya taasisi za TEFO na Shury Agri Farm Ltd.
Zephania Gideon Kang’anga, Mkurugenzi wa Shury Agri Farm Ltd, amesema taasisi yao kwa kushirikiana na TEFO inalenga kusaidia watoto yatima kutambua na kutimiza ndoto zao kupitia elimu na ujasiriamali.
Kwa upande wake, Katibu wa Asasi za Kiraia Jiji la Mbeya, Mustafa Namnenje, amepongeza juhudi za Mwasanjobe kuwekeza katika maisha ya watoto yatima, huku akiitaka jamii kuunga mkono jitihada hizo.
Mwalimu Andrew Ezekiel Wihala, mlezi wa watoto yatima, amesisitiza kuwa tukio hilo lina umuhimu wa kijamii kwani linawakumbusha Watanzania wajibu wa kuwatunza na kuwawezesha watoto waliopoteza walezi wao.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, Emmanuel Mwambelo, pamoja na Benson Thom na Deborah Emmanuel, wamezitaka taasisi na wadau kuunga mkono na kudhamini tukio hilo la kihistoria litakalogusa maisha ya we