Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA BAHATI NDINGO ALIPOKUWA AKIREJESHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBARALI

August 28, 2025

Mwanamke miaka 50 aoana na kijana wa miaka 21 baada ya penzi lao kuvutia kijiji kizima kwa mshangao

August 27, 2025

KAILIMA AFUNGA KIKAO CHA UPANGAJI WA RATIBA YA KAMPENI ZA WAGOMBEA URAIS

August 27, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • HIKI NDICHO ALICHOKISEMA BAHATI NDINGO ALIPOKUWA AKIREJESHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBARALI
  • Mwanamke miaka 50 aoana na kijana wa miaka 21 baada ya penzi lao kuvutia kijiji kizima kwa mshangao
  • KAILIMA AFUNGA KIKAO CHA UPANGAJI WA RATIBA YA KAMPENI ZA WAGOMBEA URAIS
  • Pastor akimbia baada ya mke wake kuvamia madhabahu akilia
  • MAHUNDI Atamka Hadharani: Samia na Tulia Ushindi wa Kishindo 2025
  • Jinsi ya Kumkamata Mpenzi Wako Akiwa na Mpango wa Kando Bila Stress
  • Masache Kasaka achukua fomu ya Ubunge Lupa Chunya aingia site kibabe
  • MAHUNDI: CHAMA CHA MAPINDUZI NA MPEPERUSHA BENDERA MWALUNENGE NDIYO HABARI YA MBEYA MJINI
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » MWAMBENE, MARO WAKABIDHIWA VITAMBULISHO RASMI VYA UANDISHI WA HABARI
Uncategorized

MWAMBENE, MARO WAKABIDHIWA VITAMBULISHO RASMI VYA UANDISHI WA HABARI

Mbeya YetuBy Mbeya YetuAugust 7, 2025No Comments0 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam
Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene, pamoja na mpiga picha wa zamani wa Rais, Ikulu, Fredrick Maro, wamekabidhiwa rasmi Vitambulisho vyao vya Uandishi wa Habari (Presscard) leo tarehe 07 Agosti 2025, baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria.
Zoezi hilo limefanyika katika Ofisi za Bodi zilizopo Mtaa wa Jamhuri, jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula.
Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi vitambulisho hivyo, Wakili Kipangula alibainisha kuwa Mwambene na Maro wamefuata utaratibu wa kisheria,  ikiwa ni pamoja na kujisajili, kuthibitisha taaluma zao na kuwasilisha nyaraka zilizotakiwa.
“Hili ni zoezi endelevu. Waandishi wote wa habari nchini wanatakiwa kuwa na Presscard inayotolewa na Bodi ya Ithibati ili kuendesha shughuli zao za kihabari kihalali na kuzingatia maadili ya taaluma  na Sheria,” alisema Kipangula.
Kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, kifungu cha 19 (1), mtu yeyote anayetaka kufanya kazi za kihabari ni lazima awe amesajiliwa rasmi na Bodi, kuthibitishwa na kupewa kitambulisho kinachotambulika na Serikali. Vinginevyo, mtu anayejihusisha na shughuli za kihabari bila kuthibitishwa kisheria anakuwa anatenda kosa.
Assah Mwambene, ambaye pia amewahi kuhudumu kama Mkurugenzi wa Habari katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa, ni mmoja wa Waandishi wa habari wenye uzoefu mpana katika sekta ya mawasiliano na diplomasia ya umma. Fredrick Maro pia ni mpiga picha maarufu aliyekuwa karibu na taasisi ya Urais kwa miaka kadhaa, na mchango wake umetambuliwa mara nyingi katika vyombo vya habari na kumbukumbu za taifa.
Wakati huo huo, Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari imeendelea na kampeni ya kuwasisitiza waandishi wote wanaofanya kazi katika maeneo mbalimbali kuhakikisha wanajisajili, kuthibitishwa, na kufanya kazi kwa kufuata maadili ya taaluma yao.
“Tunapenda kuona taaluma ya habari ikiheshimika, na hilo linaanza na kila mwandishi kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria. Hii inalinda hadhi ya taaluma na maslahi mapana  ya taifa,” aliongeza Wakili Kipangula.
Mpaka sasa ya waandishi wa habari  3,240 wameshajisajili, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka kutokana na mabadiliko yanayoendelea ndani ya vyombo vya habari na utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa Ithibati.
Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Mwanamke miaka 50 aoana na kijana wa miaka 21 baada ya penzi lao kuvutia kijiji kizima kwa mshangao

August 27, 2025

KAILIMA AFUNGA KIKAO CHA UPANGAJI WA RATIBA YA KAMPENI ZA WAGOMBEA URAIS

August 27, 2025

Pastor akimbia baada ya mke wake kuvamia madhabahu akilia

August 27, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025204

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024182

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 202592

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202486
Don't Miss
Video Mpya

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA BAHATI NDINGO ALIPOKUWA AKIREJESHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBARALI

By Mbeya YetuAugust 28, 20250

#mbeyayetutv

Mwanamke miaka 50 aoana na kijana wa miaka 21 baada ya penzi lao kuvutia kijiji kizima kwa mshangao

August 27, 2025

KAILIMA AFUNGA KIKAO CHA UPANGAJI WA RATIBA YA KAMPENI ZA WAGOMBEA URAIS

August 27, 2025

Pastor akimbia baada ya mke wake kuvamia madhabahu akilia

August 27, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA BAHATI NDINGO ALIPOKUWA AKIREJESHA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBARALI

August 28, 2025

Mwanamke miaka 50 aoana na kijana wa miaka 21 baada ya penzi lao kuvutia kijiji kizima kwa mshangao

August 27, 2025

KAILIMA AFUNGA KIKAO CHA UPANGAJI WA RATIBA YA KAMPENI ZA WAGOMBEA URAIS

August 27, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025204

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024182

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 202592
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.