Wakazi wa kijiji cha Marachi wamesalia kushangaa baada ya tukio la kipekee ambalo limechukuliwa na wengi kama ishara ya nguvu za kiroho za ulinzi.
Familia moja kutoka eneo hilo ilieleza jinsi walivyopata onyo lisilo la kawaida kupitia ndege mkubwa mwenye manyoya meupe yaliyong’aa na macho ya dhahabu, dakika chache kabla ya tukio baya kutokea.
Mashuhuda walisema ndege huyo alionekana kwenye paa la nyumba ya familia ya Bw. Otieno usiku wa Jumamosi, akitoa mlio wa ajabu mara tatu kisha akapaa angani.
“Tulidhani ni kisa cha kawaida,” alisema Bi. Atieno, mke wa Otieno. “Lakini dakika chache baadaye, tuliona kundi la wanaume watatu wakisogea kimyakimya kuelekea nyumbani kwetu.”
Kwa bahati nzuri, familia hiyo iliweza kupiga simu na kupata msaada wa haraka kutoka kwa majirani, na wavamizi wakashindwa kutekeleza mpango wao. Soma zaidi hapa