Sherehe ya harusi iliyotarajiwa kuwa ya furaha iligeuka kuwa sinema ya kushtua Jumamosi iliyopita katika mtaa wa Umoja, Nairobi. Waalikwa walikuwa wameketi kwa furaha wakisubiri bwana harusi na bibi harusi kuunganishwa rasmi na mchungaji, lakini ghafla hali ikabadilika.
Bibi harusi, aliyejulikana kwa jina la Carol, alipoanza kusoma viapo vyake, ghafla alisimama kidogo huku akihema kwa wasiwasi.
Kabla hajamaliza maneno, mwanamke mmoja kutoka umati aliibuka na kusema kwa sauti kubwa: “Huyo bibi harusi tayari ni mjamzito, na si mimba ya bwana harusi!”
Kauli hiyo ilileta mshangao mkubwa. Watu walibaki kimya kwa sekunde kadhaa, halafu minong’ono ikaanza kusambaa kanisani. Bwana harusi, kwa jina Brian kutoka Kayole, alionekana kushangaa na kushikwa na hasira, akimtazama Carol bila kuelewa. Bibi harusi alipata presha ya ghafla, miguu ikalegea, na akaanguka pale madhabahuni mbele ya waalikwa wote. Soma zaidi hapa