Wazo la kupata watoto mapacha limekuwa ndoto kwa wanandoa wengi, hasa wale wanaotamani familia kubwa na yenye furaha ndani ya muda mfupi.
Ingawa mara nyingi watu hufikiria kuwa mapacha hutokea tu kwa bahati au urithi wa kifamilia, kuna njia kadhaa ambazo zinaweza kuongeza nafasi ya kupata watoto mapacha bila kulazimika kufika hospitalini mara kwa mara.
Kwanza, chakula unachokula kina nafasi kubwa katika kusaidia mwili kujiandaa kupata mimba ya mapacha.
Tafiti zimeonyesha kuwa vyakula vyenye protini nyingi kama vile mayai, maziwa, samaki na nyama safi vinaweza kuchochea uzalishaji wa mayai zaidi ya moja katika mzunguko wa hedhi. Pia, vyakula vyenye folic acid kama mboga za majani, karanga na ndizi mbivu husaidia kuongeza afya ya uzazi. Soma zaidi hapa