Video inayotrend kwenye TikTok imezua maoni mengi tofauti baada ya kuonyesha sherehe ndogo ya harusi kati ya mwanamke mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka hamsini na kijana anayekadiriwa kuwa na miaka ishirini na moja, tukio lililowavutia na kuwashangaza watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii.
Katika video hiyo, wanandoa hao wanaonekana wakiwa wamependeza, wameshikana mikono huku wakitazamana kwa tabasamu la dhati, ishara kwamba penzi lao limejaa furaha na matumaini.
Watu waliokuwa wamezunguka eneo hilo walionekana kushangilia na kupiga makofi, ishara ya kuunga mkono hatua waliyochukua. Mmoja wa watumiaji wa TikTok alitoa maoni akisema, “Hii inathibitisha kuwa mapenzi ni moyo, si tarehe ya kuzaliwa.”
Mjadala ulioibuka kwenye mitandao ya kijamii umegawanya maoni. Wapo waliolipongeza tukio hilo, wakisema ni mfano wa kuthibitisha kuwa mapenzi hayana mipaka ya kiumri, na kuwa mapenzi ya kweli hujengwa na heshima, mawasiliano mazuri, na kuelewana. Wengine walionesha mshangao, wakikiri kuwa hawajazoea kuona tofauti kubwa ya umri katika ndoa, hasa pale mwanamke anapokuwa mkubwa kuliko mwanaume. Soma zaidi hapa