Mbunge Mteule wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi, amewasihi
wananchi wa Jimbo la Lupa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya kujitokeza kupiga kura oktoba 29,2025 kuhakikisha wanakipa kura za heshima Chama Cha Mapinduzi(CCM)katika ngazi zote tatu yaani Urais, Ubunge na Udiwani.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Lupa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewasihi wananchi kwenye Viwanja vya Itumbi Kata ya Matundasi kuwa ni vema wakakiamini Chama cha Mapinduzi huku ameweka bayana ajenda kuu zikiwa ni Barabara, Maji, Afya, Sekta ya Madini na Elimu.