Na. Mwandish Glascow Scotland.
Shirikisho la askari wa kike duniani na wasimamizi wa sheria duniani limeendelea na mafunzo kwa askari na wasimamizi wa sheria katika jiji la Glascow nchini Scotland huku kila mshiriki akiahidi kurudi katika taifa lake na matokeo Chanya ya maboresho katika kukabiliana na uhalifu.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi kutoka nchini Tanzania ASP Taus Salum akaeleza namna ambavyo wamejifunza katika matumizi ya data kuchunguza na kutatua uhalifu huku akiahidi Kwenda kupeleka elimu hiyo ili kuongeza ufanisi katika kupambana na uhalifu unaendana na mabadiliko ya teknolojia.
Ameongeza kuwa katika mafunzo hayo, wameona mataifa yaliyofanikiwa katika matumizi ya sayansi data katika kudhibiti uhalifu ambapo amesema kuwa watakwenda kuboresha na kutumia elimu hiyo kudhibiti uhalifu ambao upo kasi na maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani.
Kwa upande wake Kamishna wa Uhamiaji vibali vya Ukaazi na Viza na Pasi kutoka Idara ya uhamiaji nchini Tanzania (CI) Angela Shija amebanisha kuwa wamejifunza namna ya kupamabana na wahamiaji haramu na matumizi sahihi ya teknolojia katika kuwabaini wahalifu na wahamiaji haramu wanaoingia nchini bila kufuata utaratibu.
Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt Deborah Magiligimba yeye akaweka wazi namna ambavyo wamejifunza masuala ya Polisi jamii na matumizi sahihi ya mifumo ya Tehama huku akifafanua zaidi namna walivyo furahishwa na mfumo wa Polisi kata wanavyofanya kazi kwa kushirikiana na Jamii nchini Tanzania.
Nae Mrakibu wa Polisi kutoka nchini Nigeria (SP) Funmi Akinsanmi akafafanua kuwa wamejifunza namna ya kutenga muda wa kazi na mambo binafsi ili kujiwekea mizani sawa ambayo italeta ufanisi katika kazi zao za kila siku.
Kamishna Msaidizi wa uhamiaji ambaye ni mkuu wa chuo cha kikanda (TRITA) Hoja Mahiba akabainisha kuwa mafunzo hayo pia yamewajenga na kusisisitiza ushiriki wa maafisa wa kike kushiriki katika operesheni mbalimbali za kulinda amani katika mataifa yenye changamoto.