Katika kijiji kidogo kilichopo Tarime, aliishi kijana aitwaye Benedicto. Alizaliwa katika familia ya kimasikini sana, familia ambayo mara nyingi ililala njaa na kuamka bila matumaini ya kesho. Wazazi wake walikuwa wakulima wadogo wa mahindi na maharagwe, lakini kilimo chao hakikuwahi kuwaletea chochote cha maana zaidi ya chakula cha kutosheleza siku chache. Benedicto alikua akichunga ng’ombe na kondoo wa watu ili kupata pesa ndogo za kujikimu.
Moyo wa Benedicto ulikuwa na kiu ya mafanikio. Mara nyingi alipokuwa akikaa juu ya kilima, akitazama migodi ya madini inayochimbwa maeneo jirani, alijiambia: “Siku moja nami nitakuwa tajiri mkubwa, sitateseka kama sasa.” Kauli hiyo aliijirudia kila siku, na ndoto yake ikawa kama mwanga wa kumvuta mbali na maisha ya umaskini.
Miaka ilipozidi kusonga, Benedicto alipata nafasi ya kujiunga na vijana waliokuwa wakichimba madini kwa njia ya kienyeji. Mwanzoni hakuwa na vifaa, bali alikuwa msaidizi wa wachimbaji wengine. Lakini bidii yake na uaminifu vilimfanya aaminiwe. Hatimaye akajikusanyia mtaji mdogo wa kununua mashine ya kuchimba madini.
Kwa bahati nzuri, kazi yake ilimletea mafanikio makubwa. Aligundua sehemu yenye mawe yenye thamani kubwa. Ndani ya muda mfupi akawa tajiri wa ghafla. Aliweza kujenga nyumba nzuri mjini Tarime, kununua magari ya kifahari, na kusaidia familia yake. Vijana wa kijiji walimwona kama kioo cha kuigwa, na wazee walimbariki kama kijana shupavu aliyebadili historia ya familia yake. Soma zaidi hapa