Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi wa tukio la
mauaji ya aliyekuwa Mwanachuo wa mwaka wa kwanza katika Chuo
Kikuu cha Mzumbe ndaki ya Mbeya kitivo cha sheria aitwaye Shairose
Michael Mabula [21].
Awali mnamo tarehe 14 Septemba, 2025 Baba mzazi wa marehemu
aitwaye Dkt Michael Mabula alifika kituo kikuu cha Polisi Mbeya na kutoa
taarifa ya kupotea kwa binti yake aitwaye Shairose Mabula ambapo
jalada la uchunguzi lilifunguliwa na kuanza ufuatiliaji ili kumpata. mnamo
tarehe 16 Septemba, 2025 saa 5:00 usiku huko Mtaa wa Morovian uliopo
Kata ya Isyesye Jijini Mbeya ilipokelewa taarifa ya ajali ya moto ambapo
Askari walifika eneo la tukio na kukuta kibanda kinateketea kwa moto.
Baada ya uchunguzi ilibainika kuna mwili wa mtu mmoja jinsia ya kike
unaugua ambaye kwa wakati huo hakuweza kutambulika.
Mwili wa marehemu ulichukuliwa na kuhifadhiwa Hospitali ya Rufaa
Kanda Mbeya na baada ya uchunguzi wa kitabibu na kuhusisha ndugu
ilibainika kuwa mwili huo ni wa Shairose Mabula aliyekuwa anatafutwa
baada ya kuripotiwa kupotea.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi wa kina
ikiwemo uchunguzi wa kisayansi ili kubaini na kutambua mwili wa
marehemu na kuwakamata waliohusika na mauaji haya. Aidha, Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa
zitakazofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa azitoe. Pia, Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mbeya linaendelea kutoa rai kwa jamii kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mkononi na kusababisha madhara makubwa kama
mauaji.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.
Trending
- Mtoto wa Jenista Mhagama Aibua Hisia Kali, Asema Mama Yake Hana Deni
- RAIS SAMIA KWA UCHUNGU MSIBANI – ”TUTALIMISI TABASAMU LAKE –
- MADEREVA BODABODA MKOANI IRINGA WALAANI VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI.
- MAHAFALI YA 23 YA TAASISI YA UHASIBU TIA KAMPASI YA MBEYA, RC MALISA AWAALIKA WAWEKEZAJI MKOANI MBEYA.
- Ilinde biashara dhidi ya husda na mikosi
- Fanya hivi kuvutia fursa mpya za kazi
- WASHINDI WA MAWAZO BUNIFU WANAZUONI TAASISI YA UHASIBIU TIA KUFANYA ZIARA YA KIMAFUNZO NJE YA NCHI
- “KUNUNA MWISHO – MWALUNENGE AWAPA MOTISHA VIJANA WA KIWIRA: PESA IPO, CHANGAMKIA FURSA”

