Leo nimekuja mbele yenu nikiwa na ari na msisimko wa kweli. Nitumieni nikafanye kazi kwa ajili yenu na kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo la Mbeya Mjini.
Nataka tushirikiane kubadilisha Mkoa wa Mbeya – tubebe pamoja ajenda ya maendeleo kwa tabasamu na mshikamano. Nina afya, nina nguvu, nina ujuzi na ubunifu. Nina dhamira thabiti ya kusimamia na kulinda maslahi ya wananchi wa Mbeya.
Nikiwa mgombea wa Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), naomba tushirikiane katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29. Naomba kura zenu kwa ajili ya Rais wetu mpendwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kura kwa ajili yangu kuwa Mbunge wenu, na kura kwa Diwani wa CCM.
Tukiwa pamoja, tutaendelea kusonga mbele. Nitumieni nikafanye kazi.
Asanteni sana.