Mbunge mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ameibukia Soko la Uhindini lililopo Kata ya Chokaa Wilaya ya Chunya Mkoani kwa lengo la kukutana na Wanawake wajasiriamali wanaofanya biashara katika Soko hilo.
Aidha amewatia moyo na kuwahimiza kumiliki uchumi wao sanjari na kujiunga pamoja ili waweze kunufaika na mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri.
Aidha Mahundi ametumia fursa hiyo kuzisaka kura za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Mbunge na Diwani ili kuendeleza maendeleo nchini.