Zaidi ya wanaume 1000 kutoka katika mji wa Tunduma mkoani Songwe wamefunga Barabara kwa saa kadhaa wakifanya matembezi ya aina yake na kuwaacha watu midomo wazi barabarani wakiadhimisha mwaka mmoja wa muungano wa kikundi chao maalum Cha kijamii chenye lengo la kuinuana na kusaidiana wao kwa wao.
Mwenyekiti wa kikundi hicho Herode Jivava anasema waliamua kuanzia kikundi hicho ili kumkomboa mwanaume na aibu ambazo amekuwa akikumbana nazo pindi linapotokea jambo la furaha ama huzuni hivyo wao wapo kwaajili ya kumuinua na kumrejeshea heshima mwanaume huyo.