Leo kupitia kampeni ya GESI YENTE iliyoandaliwa na Oryx Gas Tanzania, washindi mbalimbali kutoka mkoa wa Mbeya wamekabidhiwa zawadi zao walizojishindia baada ya kushiriki kwenye kampeni hiyo.
Zawadi zilizotolewa ni pamoja na pikipiki, majiko ya gesi, baiskeli, helmeti, kofia, na zawadi nyingine nyingi — zote zikilenga kuwazawadia wateja waaminifu wa Oryx Gas wanaojaza mitungi yao kwa usalama na uhakika.
Kampeni hii maalum ya “Gesi Yente – Mambo ni Yente” ilizinduliwa tarehe 13 Agosti 2025 na itaendelea hadi 13 Oktoba 2025, ikitoa fursa kwa wateja wote wa Oryx Gas kujishindia zawadi kemkem kwa kujaza mitungi yao katika vituo rasmi vya kampuni hiyo.
💬 Oryx Gas Tanzania inawahamasisha wateja wote kuendelea kushiriki kampeni hii kwa kujaza mitungi yao ili nao wapate nafasi ya kujishindia zawadi kabla ya kampeni kumalizika.
🔥 Gesi Yente – Mambo ni Yente!
#OryxGas #GesiYente #MamboNiYente #Mbeya