WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha ustahimilivu wa Taifa dhidi ya majanga, kupitia utekelezaji wa sera, sheria, mikakati na miradi mbalimbali
Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuendelea katika kujenga ustahimilivu wa jamii dhidi ya maafa, tutaokoa maisha, mali, na rasilimali za taifa letu.
Amesema hayo leo Jumatatu (Oktoba 13, 2025) wakati alipotoa tamko katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kupunguza madhara ya maafa, katika ukumbi wa mikutano wa City Park Garden jijini Mbeya.