Jina langu ni Miriam, na hadi leo nikikumbuka mateso niliyopitia mikononi mwa mtu niliyemwamini, moyo wangu hujaa maumivu na faraja kwa wakati mmoja. Nilikuwa katika uhusiano wa miaka minne na mwanaume niliyempenda sana.
Nilimsaidia kifedha, kihisia, na hata nilimkopesha pesa ili aanze biashara. Lakini baada ya kujinyanyua, alinitupa kando kana kwamba sikuwa na maana tena. Aliniambia wazi kuwa hangeweza kuendelea kuwa na “mwanamke asiye na thamani,” maneno ambayo yaliniumiza zaidi ya kisu moyoni.
Siku moja aliniita kwenye hafla yake ya “uzinduzi wa biashara,” nikafika nikijua ni mwanzo wa kitu kipya kwetu, kumbe ilikuwa ni harusi yake na mwanamke mwingine. Nilihisi dunia imenigeuka. Nililia hadi macho yakavimba, nikajifungia nyumbani kwa siku nyingi nikiwa sina hamu ya kula wala kutoka nje. Nilipoteza marafiki, kujiamini kukatoweka, na nilianza hata kuamini kuwa labda nililaaniwa. Soma zaidi hapa