Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika Jumatano, Oktoba 29, 2025.
✅ Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni.
✅ Vituo vya magereza vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri.
✅ Kila mpiga kura anatakiwa kufika kituoni na kadi yake ya kupigia kura.
✅ Waliopoteza kadi wataruhusiwa kutumia NIDA, leseni au pasi ya kusafiria endapo jina lipo kwenye daftari la wapiga kura.
🗓️ Taarifa hii imetolewa na Ms. Anamary Joseph Mbunga, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbeya Mjini – tarehe 19 Oktoba 2025.