Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Beno Malisa ametoa wito kwa wafanyabiashara kulipa leseni za biashara kwa wakati, ili kuiwezesha Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo.
RC Malisa ameyasema hayo wakati akikabidhi madawati 1,000 kwa shule 15 za msingi jijini Mbeya, yaliyotengenezwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Mkurugenzi wa Jiji, Justine Kijazi, amesema zaidi ya milioni 130 zimetumika kutengeneza madawati na meza kwa shule mbalimbali.

