Nilikuwa nikiamini kwamba ndugu ni ngao ya damu, watu ambao hata dunia ikinigeuka, wao watabaki upande wangu. Kwa muda mrefu nilikuwa karibu sana na kaka yangu mkubwa. Tulikua pamoja, tukagawana siri, na kila nilipopata mafanikio, nilihakikisha anafaidika pia.
Lakini polepole nilianza kuhisi mambo hayapo sawa. Kila mara nilipopanga jambo muhimu, lilikuwa likiharibika ghafla bila sababu. Nilijaribu kuamini ni bahati mbaya, lakini matukio yalizidi kujirudia.
Nilianza kupata ndoto za ajabu. Wakati mwingine nilimuona kaka yangu akiwa ananiangalia kwa macho makali, au akinigeukia akiwa amevaa nguo nyeusi. Nilipoamka, nilihisi hofu isiyoelezeka.
Nilijaribu kupuuzia, lakini siku moja niliamka nikihisi kizunguzungu kikali na mwili mzima ukawa dhaifu kana kwamba nimechoka kufanya kazi ngumu usiku kucha. Nilipokwenda hospitali, madaktari hawakuona tatizo lolote.
Wakati huo ndipo nilipoanza kufikiria mambo ya kiroho. Nilianza kuunganisha matukio yaliyokuwa yanatokea karibu nami miradi yangu kuharibika dakika za mwisho, marafiki kuanza kunitenga bila sababu, na hata mke wangu kunilalamikia kuwa usiku naongea maneno ya ajabu nisiyoyajua. Hapo ndipo nilipoanza kufikiri kuna kitu zaidi ya macho kinachoendelea. Soma zaidi hapa

