Sikuwa nimewahi kufikiria kwamba siku moja ningechagua ndoa yangu badala ya kazi niliyopigania kwa miaka mingi. Nilikuwa nafanya kazi katika kampuni kubwa mjini, mshahara mzuri, marupurupu mazuri, na heshima kazini. Lakini nyuma ya mafanikio hayo, ndoa yangu ilikuwa ikivunjika taratibu.
Mume wangu alianza kulalamika kwamba sina muda wa familia. Kila siku nilikuwa ninarudi usiku, nikiwa nimechoka, sina nguvu hata ya kuzungumza naye. Mara nyingi, chakula cha usiku kilikuwa kimpoa, na mazungumzo yetu yakawa mabishano badala ya upendo. Nilidhani ana wivu wa mafanikio yangu, lakini baadaye niligundua alikuwa analia kwa upweke.
Siku moja nilipofika nyumbani, nilimkuta amepanga mizigo yake. Aliniambia kwa sauti ya upole, “Sina tatizo na kazi yako, ila nimeanza kuhisi sina mke tena.” Nilihisi kama moyo wangu umepasuka. Nilimlilia, nikimwomba asiondoke. Hiyo usiku sikulala kabisa. Nilitambua kuwa nimepoteza kitu muhimu kuliko kazi amani ya familia yangu.
Siku iliyofuata, nilienda kazini nikiwa na macho mekundu. Nilikaa ofisini nikitazama kompyuta bila kufanya kazi. Ndani yangu kulikuwa na vita kubwa kazi au ndoa? Nilikaa kimya kwa muda, kisha nikaandika barua ya kujiuzulu. Ilikuwa maamuzi magumu zaidi maishani mwangu, lakini nilihisi ni lazima nifanye hivyo.
Niliporudi nyumbani na kumwambia mume wangu, alinishika mkono na kulia. Alisema, “Sikuwahi kufikiria utaweza kufanya hivi kwa ajili yetu.” Tulikumbatiana kwa muda mrefu, na kwa mara ya kwanza baada ya miezi mingi, nilihisi amani ndani ya nyumba yangu. Lakini mambo hayakuwa rahisi baada ya hapo nilianza kuhisi wasiwasi, nikijiuliza kama nilifanya uamuzi sahihi. Soma zaidi hapa

