Huko Katavi, eneo lenye utajiri wa madini na ardhi, ilikuwa nyumbani kwa Juma, kijana mwenye bidii lakini aliyekandamizwa na mzigo wa umaskini. Juma alijaribu kila kazi aliyoweza kupata, kuanzia vibarua vya mashamba hadi ulinzi wa usiku, lakini juhudi zake zote hazikuweza kuutoa mguu wake kwenye tope la umasikini.
Alipanga chumba kimoja kidogo, maisha yake yaliendeshwa kwa mkono na mdomo, na ndoto zake za kusaidia familia yake na kuboresha maisha yake zilionekana kuwa mbali sana. Kila asubuhi ilikuwa pambano jipya la kutafuta njia ya kujikimu.
Kwa miaka kadhaa, Juma alikuwa akijaribu bahati yake katika michezo ya kubashiri (betting). Alitumia kiasi kidogo cha pesa alichokipata kubashiri mechi za soka, akitumaini siku moja atashinda kiasi kikubwa ambacho kingebadili maisha yake. Hata hivyo, mara nyingi alikuwa akipoteza.
Alikuwa akikaribia kushinda, lakini daima kuna mechi moja au mbili zilimharibia mkeka wake. Hali hii ilimfanya ajihisi kukata tamaa na alishawahi kufikiria kuacha kabisa.
Siku moja, Juma alikuwa amekaa kwenye kiti cha vinywaji na marafiki zake, akisimulia jinsi anavyokosa kwa pointi chache sana katika betting zake. Mzee mmoja, ambaye alikuwa amesikiliza kwa kimya, alimuita Juma kando. Soma zaidi hapa

