Salma alikuwa mwanamke mrembo na mwenye tabasamu la kuvutia, akiishi Dar es Salaam, jiji lenye shamrashamra nyingi. Alikuwa ameolewa na Ramadhani, mfanyabiashara mchapakazi, na walibarikiwa kuwa na watoto wawili warembo. Kwa macho ya wengi, maisha yao yalikuwa picha kamili ya furaha. Walakini, nyuma ya milango iliyofungwa, Salma alibeba mzigo mzito moyoni mwake.
Changamoto kubwa iliyomkabili ilikuwa kwenye eneo muhimu la ndoa yao: kutofurahia tendo la ndoa. Kila alipojaribu kuwa karibu na mumewe, alihisi kama anatimiza wajibu tu, bila hisia yoyote ya shauku au utamu. Hali hii ilianza taratibu, kama kivuli kidogo, lakini baada ya muda, ilikua na kuwa mwamba mkubwa katikati ya mapenzi yao.
Ramadhani alijitahidi kumfanya mkewe afurahi; alimpeleka likizo, alimnulia zawadi, na alizungumza naye kwa upole. Lakini kadiri muda ulivyokwenda, Ramadhani alianza kuhisi kutengwa na kuchanganyikiwa, akidhani labda amemchukiza mkewe.
Mazungumzo yao yalianza kuwa machache, na hata tabasamu la Salma lilikuwa likififia. “Kuna nini Salma? Sioni tena furaha machoni pako,” Ramadhani aliwahi kumuuliza kwa uchungu, jambo ambalo liliongeza tu maumivu ya Salma. Alijua tatizo lilianzia kwake, lakini hakuwa na ufumbuzi.
Salma alizunguka kwa madaktari wa kawaida, wataalamu wa saikolojia, na hata wataalamu wa lishe, akitafuta suluhisho la kisayansi. Kila utambuzi ulikuwa nafuu ya muda, lakini shida hiyo ilirudi tena na kumsumbua zaidi. Matumaini yake yalikuwa yamepungua, na alianza kukubali hali hiyo kama “hatima” yake. Soma zaidi hapa

