Katikati mwa jiji la Dar es Salaam, Ilala, aliishi Beka, kijana aliyefaulu masomo yake kwa kiwango cha juu kabisa katika mojawapo ya Vyuo Vikuu vinavyoheshimika nchini, akihitimu na shahada ya Uhazibu (Accounting) kwa daraja la kwanza, First Class Honours. Kwa akili yake kali, aliamini kwamba kazi nzuri ingemngoja mara tu atakapomaliza masomo.
Baada ya sherehe ya mahafali, Beka alirudi Ilala na kuanza mchakato wa kutuma maombi ya kazi kwa bidii kubwa. Alikuwa na sifa zote: ufaulu bora, ujuzi wa kompyuta, na ari ya kufanya kazi. Alituma maombi katika makampuni makubwa na madogo, akifanya usaili mmoja baada ya mwingine.
Lakini kila mara, jibu lilikuwa lile lile: “Samahani, tumepata mtu anayefaa zaidi.”
Wiki zikapita, zikageuka miezi, na miezi ikawa mwaka mmoja, kisha miaka miwili. Beka alibaki nyumbani, akitegemea wazazi wake na wazo la kuanzisha biashara likawa gumu kutokana na ukosefu wa mtaji. Aliona wenzake wa darasa, waliokuwa na ufaulu wa kawaida, wakipata kazi kubwa na kufanikiwa, lakini yeye – mwenye ufaulu bora alibaki nyuma. Soma zaidi hapa

