Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Aga Khan Zaanzisha Ushirikiano wa Kuboresha Huduma za Afya

February 6, 2026

Shule ya Sekondari Utengule Usangu, H

February 6, 2026

Mradi wa Barabara Mlima Nyoka Wamfikisha MCC ASAS, Ataka Kero za Wananchi Zitokomee

February 5, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Aga Khan Zaanzisha Ushirikiano wa Kuboresha Huduma za Afya
  • Shule ya Sekondari Utengule Usangu, H
  • Mradi wa Barabara Mlima Nyoka Wamfikisha MCC ASAS, Ataka Kero za Wananchi Zitokomee
  • Mradi wa Soko la Matola Wakwama, Meya na MNEC Wakanusha Kukamilika Mei
  • JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA
  • Halmashauri Yaipongeza Mbeya UWSA Kwa Mradi wa Maji, Asema Utakuza Uwekezaji
  • Mpango wa Maendeleo 2026/27: Kasaka Apongeza Mafanikio, Aomba Maboresho
  • Msafara Wasimama Soweto, Mbunge Mwalunenge Aamuru TANROADS Kuondoa Dimbwi la Miaka 3 Mara Moja
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » Teknolojia Mpya ya Kukaushia Mpunga Yazinduliwa: Dryer ya Tani 8 kwa Saa 4 Yaonyesha Uwezo Wake
Video Mpya

Teknolojia Mpya ya Kukaushia Mpunga Yazinduliwa: Dryer ya Tani 8 kwa Saa 4 Yaonyesha Uwezo Wake

Mbeya YetuBy Mbeya YetuNovember 28, 2025No Comments17 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Wadau wa kilimo kutoka taasisi za Serikali na sekta binafsi wamepatiwa mafunzo juu ya matumizi ya mashine za kisasa za kukaushia na kupima unyevu wa mazao ya nafaka, katika warsha iliyoandaliwa na Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na JICA jijini Mbeya.

Warsha hiyo imefanyika tarehe 26 Novemba 2025 katika shamba la Raphael Group Ltd, ambapo mashine ya Batch Circulating Dryer yenye uwezo wa kukaushia hadi tani 8 za mpunga ndani ya saa 4 imeoneshwa kwa vitendo. Teknolojia hii inatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa upotevu wa mazao baada ya mavuno.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mhandisi Sekela Mwakihaba kutoka Idara ya Zana za Kilimo na Uongezaji Thamani alisema ushiriki wa wadau unaonesha dhamira ya Serikali ya awamu ya sita kuboresha mnyororo wa thamani wa mazao na kupunguza uharibifu wa nafaka wakati wa uvunaji. Alibainisha pia kuwa Serikali inaendelea kusukuma matumizi ya teknolojia kupitia utekelezaji wa Agenda 10/30 ili kuongeza tija na kipato cha wakulima.

Kwa upande wake, Meneja wa Uzalishaji wa Raphael Group Ltd – Kituo cha Uyole, Bw. Maisha Ambangile, alisema mashine hiyo itasaidia wakulima kupata nafaka kavu kwa ubora wa soko na kwa muda mfupi, huku gharama ya mashine moja ikiwa takriban shilingi milioni 188.

Warsha hiyo imeratibiwa na JICA kwa kushirikiana na kampuni za YAMAMOTO (watengenezaji wa mashine za kukaushia nafaka) na Kett Electric Laboratory (watengenezaji wa mashine za kupima unyevu), ikiwakutanisha maafisa wa Serikali, wataalamu wa JICA, wamiliki wa mitambo ya ukavu na wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Aga Khan Zaanzisha Ushirikiano wa Kuboresha Huduma za Afya

February 6, 2026

Shule ya Sekondari Utengule Usangu, H

February 6, 2026

Mradi wa Barabara Mlima Nyoka Wamfikisha MCC ASAS, Ataka Kero za Wananchi Zitokomee

February 5, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025330

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024226

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025139
Don't Miss
Video Mpya

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Aga Khan Zaanzisha Ushirikiano wa Kuboresha Huduma za Afya

By Mbeya YetuFebruary 6, 20261

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Aga Khan Health Service Tanzania zimeingia katika makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati unaolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania. Akizungumza jijini Mbeya, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji, alisema ushirikiano huo utawezesha kubadilishana ujuzi na uzoefu kati ya sekta ya umma na binafsi kwa manufaa ya wananchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Aga Khan Health Service Tanzania, Sisawo Konteh, alisema makubaliano hayo yataimarisha huduma za kliniki, kujenga uwezo wa watumishi, kuboresha mifumo ya ubora na kusaidia hospitali hiyo kupata ithibati. Ushirikiano huo pia utahusisha mafunzo, tafiti na kuendeleza huduma bingwa ikiwemo saratani na magonjwa ya moyo, pamoja na kukuza utalii wa tiba katika mkoa wa Mbeya.

Shule ya Sekondari Utengule Usangu, H

February 6, 2026

Mradi wa Barabara Mlima Nyoka Wamfikisha MCC ASAS, Ataka Kero za Wananchi Zitokomee

February 5, 2026

Mradi wa Soko la Matola Wakwama, Meya na MNEC Wakanusha Kukamilika Mei

February 5, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Aga Khan Zaanzisha Ushirikiano wa Kuboresha Huduma za Afya

February 6, 2026

Shule ya Sekondari Utengule Usangu, H

February 6, 2026

Mradi wa Barabara Mlima Nyoka Wamfikisha MCC ASAS, Ataka Kero za Wananchi Zitokomee

February 5, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025330

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025252

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024226
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.