Na WAF, Dar es Salaam.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kuwatibu watu 760 wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu ambapo shilingi Bilioni 6.7 zimetengwa kwa kazi hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26
Hayo yameibainishwa na Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa Desemba 8, 2025 alipokuwa akizungumza na watumishi wa Sekta ya Afya ngazi ya Wizara waliopo mkoa wa Dar es Salaam kwenye kikao kazi kilichofanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Kutokana na faida kubwa iliyopatikana kwa mwaka 2024/25 ambapo jumla ya wagonjwa 677 walinufaika kwa huduma za kibobezi kama kupandikizwa Uloto watoto wenye Sikoseli, Kupandikizwa figo, upasuaji wa moyo, uapndikizaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto, matibabu ya Saratani, upandikizaji wa nyonga, Rais Samia ameridhia kuwa na bajeti husika,” amefafanua Waziri Mchengerwa.
Waziri Mchengerwa amesema Rais Samia anadhamira ya dhati ya kuboresha Afya za wananchi kwakuhakikisha kila mwananchi uhitaji wa huduma za kibingwa anapata huduma hizo pasipo na kikwazo cha fedha. @wizara_afyatz @mohamed_mchengerwa

