DKT TULIA ACKSON:”Kwanza kabisa nichukue fursa hii kutoa pole kwa dhati. Sisi ni sehemu ya wananchi ambao tuliathirika na tukio lililotokea, na kama ilivyoelezwa vizuri na Sheikh wa Mkoa, sitarudia kwa kirefu. Lakini nitoe pole zangu za dhati kwa wananchi wenzangu wa Mbeya, Uyole, na Watanzania wote kwa ujumla, kufuatia tukio lililolikumba Taifa letu tarehe 29 Oktoba”.
”Wakati huohuo, baada ya dua na maelezo yaliyotolewa, nitoe pole pia kwa wananchi wenzetu waliopoteza maisha, na niwatakie uponaji wa haraka wale wote waliojeruhiwa.
Nichukue fursa hii pia, Mheshimiwa Waziri Mkuu, kukukaribisha mkoani Mbeya, lakini kwa ziara hii maalum, nitoe pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa changamoto iliyotokea, ambayo pia imekupa fursa ya kutembelea miundombinu mbalimbali ya umma na mali za wananchi zilizopata athari”.

