Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA

February 4, 2026

Halmashauri Yaipongeza Mbeya UWSA Kwa Mradi wa Maji, Asema Utakuza Uwekezaji

February 4, 2026

Mpango wa Maendeleo 2026/27: Kasaka Apongeza Mafanikio, Aomba Maboresho

February 4, 2026
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA
  • Halmashauri Yaipongeza Mbeya UWSA Kwa Mradi wa Maji, Asema Utakuza Uwekezaji
  • Mpango wa Maendeleo 2026/27: Kasaka Apongeza Mafanikio, Aomba Maboresho
  • Msafara Wasimama Soweto, Mbunge Mwalunenge Aamuru TANROADS Kuondoa Dimbwi la Miaka 3 Mara Moja
  • CCM Miaka 49: Mbunge wa Mbarali Akabidhi Mashuka Kituo cha Afya Utengule
  • Dkt. Tulia Ackson Atoa Msaada wa Vifusi Roli 10 kwa Ukarabati wa Barabara ya Chanyasi
  • TGNP na CARE Watoa Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa Jamii Mbeya
  • JUMUIYA YA WAZAZI CCM YAFUNGUA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 KWA MATEMBEZI YA AMANI โ€“ MBEYA MJINI
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home ยป JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA
Habari za Kitaifa

JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuFebruary 4, 2026No Comments4 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) ameshiriki Mkutano wa 67 wa Mawaziri wa Afya kutoka nchi 9 wanachama za Jumuiya ya Afya ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (ECSA-HC) unaofanyika Ezulwini, Ufalme wa Eswatini tarehe 2-3 Februari, 2026.

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo umejadili mikakati ya kuimarisha mifumo ya afya ya nchi wanachama wa ECSA-HC, hususan kwa kuzingatia mabadiliko yanayoendelea duniani kote yaliyopelekea kupungua au kusitishwa kabisa kwa upatikanaji wa fedha za kufadhili miradi ya afya kutoka kwa wafadhili waliozoeleka.

Katika hotuba akifungua Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi wa ECSA-HC, Dkt. Kikwete alitoa rai kwa nchi hizo kuwa wabunifu katika kubuni na kutafuta vyanzo mbadala vya rasilimali za kifedha ili kuhakikisha kuwa miradi iliyokwishaanza kutekelezwa haitetereki au kufa kutokana na kukoma kwa fedha za wafadhili. “Kama Serikali huwezi kuwaambia wananchi kuwa tunasitisha huduma za afya kwa sababu wafadhili wameacha kutoa fedha. Hapana. Ni wajibu wenu kama watunga Sera kuumiza vichwa na kufanya juu chini kutafuta vyanzo mbadala vya fedha ili wananchi waendelee kupata huduma wanazostahili”, alieleza Dkt. Kikwete.

Alitumia pia fursa hiyo kutoa uzoefu wake jinsi walivyowahi kukabiliana na changamoto za aina hiyo wakati wa uongozi wake ambapo moja ya mbinu walizobuni ni kuimarisha ushirikiano wa kikanda baina ya nchi za Afrika ili kuongeza uhimilivu wa mifumo ya afya, ikiwemo uamuzi wa nchi za ukanda huu kufanya manunuzi ya pamoja ya jumla kwa bei nafuu (bulk-procurement) ya dawa, vifaa tisa na vitendanishi badala ya kila nchi kununua vifaa hivyo kivyake.

Rais Mstaafu Dkt. Kikwete alitumia pia fursa hiyo kueleza washiriki hao hatua kubwa za mafanikio zilizopigwa na Tanzania chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya. Akitoa mfano, alieleza namna ushirikiano wa karibu kati ya Serikali ya Tanzania na wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali, ikiwemo Taasisi ya JMKF, ulivyoweza kushusha kiwango cha vifo vya wakinamama wanaojufungua kutoka vifo 560 kwa kila kinamama 100,000 wanaojifungua hadi kufikia vifo 104 na kuifanya Tanzania kuwa nchi inayoongoza barani Afrika katika kutimiza lengo la Umoja wa Mataifa la SDG 3.1 linalozitaka nchi zote duniani kushusha kiwango hicho hadi kufikia vifo 70 ifikapo mwaka 2030.

Akitoa mfano wa umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali mashirika binafsi katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya katika ngazi ya jamii, Dkt. Kikwete alieleza namna JMKF inavyotoa huduma za kliniki inayotembea (mobile outreach) kwa kinamama wajawazito wanaoishi maeneo ya mbali na vituo vya afya na magumu kufikika katika Wilaya za Uyui na Sikonge, Mkoani Tabora.

Kwa mujibu wa Taasisi ya JMKF, Mradi huo unaojulikana kama Jamii Salama umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga mkoani Tabora ambapo hadi sasa umewagusa zaidi ya wakina mama 1,500 kwa kuwapatia huduma za kliniki, ikiwemo huduma ya ultrasound, tiba ya malaria, pamoja na kuwafikia watoto wa shule zaidi ya 3,200 kwa elimu ya afya ya kinywa na malaria.

Kwa upande mwingine, Rais Mstaafu Dkt. Kikwete aliongoza washiriki wa Mkutano huo kuonana na Mfalme Mswati III wa Eswatini ambaye aliahidi kupokea ripoti itakayotokana na majadiliano ya Mkutano huo na kuifikisha kwa Viongozi wenzake wa nchi wanachana wa ECSA-HC na Jumuiya nyingine za Kikanda.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

TGNP na CARE Watoa Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa Jamii Mbeya

January 31, 2026

JUMUIYA YA WAZAZI CCM YAFUNGUA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 KWA MATEMBEZI YA AMANI โ€“ MBEYA MJINI

January 30, 2026

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Bi. Erica Yegella, Atoa Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita Siku 100

January 29, 2026

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025329

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025251

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024226

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025139
Don't Miss
Habari za Kitaifa

JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA

By Mbeya YetuFebruary 4, 20264

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa…

Halmashauri Yaipongeza Mbeya UWSA Kwa Mradi wa Maji, Asema Utakuza Uwekezaji

February 4, 2026

Mpango wa Maendeleo 2026/27: Kasaka Apongeza Mafanikio, Aomba Maboresho

February 4, 2026

Msafara Wasimama Soweto, Mbunge Mwalunenge Aamuru TANROADS Kuondoa Dimbwi la Miaka 3 Mara Moja

February 4, 2026
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

JK KWA MFALME MSWATI III KUJADILI UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA AFYA KWA NCHI WANACHAMA WA ECSA

February 4, 2026

Halmashauri Yaipongeza Mbeya UWSA Kwa Mradi wa Maji, Asema Utakuza Uwekezaji

February 4, 2026

Mpango wa Maendeleo 2026/27: Kasaka Apongeza Mafanikio, Aomba Maboresho

February 4, 2026
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025329

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025251

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024226
© 2026 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.