Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Bahati Ndingo, amegawa jezi, sufuria, majiko ya gesi pamoja na sabuni kwa wananchi na vikundi mbalimbali vya vijana katika Kata ya Utengule Usangu, wilayani Mbarali, mkoani Mbeya.
Msaada huo umetolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kuzaliwa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika kiwilaya, yakilenga kuimarisha michezo, matumizi ya nishati safi na ustawi wa jamii.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge Ndingo amesisitiza umuhimu wa vijana kukuza vipaji vyao, akibainisha kuwa michezo, hususan soka, ni ajira. Aidha, ametangaza mpango wa kuanzisha mashindano ya soka yajulikanayo kama “Bahati Ndingo Cup” baada ya msimu wa mavuno.

