Author: Mbeya Yetu

Ikiwa ni msimu wa tano tangu kuanzishwa kwa Tulia Trust Uyole Cup leo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Beno Malisa amezindua rasmi msimu wa Tano wa 2025 akiwataka wananchi kutofanya vurugu ili washuhudie vipaji kutoka Jiji la mbeya. Kwa upande wake Jaqline Boazi meneja wa Tulia Truss ameeleza namna wananchi wanavyonufahika na timu 35 kushiriki huku kaimu mwenyekiti wa wa chama cha mpira mkoa wa Mbeya akieleza namna matarajio yao ya kupata vipaji mbalimbali vya mpira.

Read More

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprsca Mahundi, amewatoa hofu wananchi kuwa Serikali inaendelea kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata huduma bora za mawasiliano hasa maeneo ya vijijini. Katika kutekeleza hilo, kata ya Mkwamba iliyopo mkoani Rukwa yenye jumla ya vijiji vinne—Swaila, Tambaruka, Itindi na Lyele—imepata mafanikio makubwa kupitia miradi ya Serikali inayolenga kuboresha mawasiliano. Kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Serikali imefanikiwa kujenga minara ya mawasiliano kwa kushirikiana na makampuni ya mawasiliano ya VODACOM na HALOTEL. Mnara wa Vodacom umejengwa katika Kijiji cha Tambaruka kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali (DTP), huku mnara wa Halotel ukijengwa…

Read More

Bwana Rémy Rioux, Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AfD), akizungumza mbele ya wajumbe wa Mkutano wa siku mbili wa Bodi ya Taasisi ya Ubia wa Elimu Duniani (Global Partnership for Education – GPE) unaofanyika mjini Paris, Ufaransa, leo tarehe 3 Juni 2025, chini ya uenyekiti wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Mkutano huo umewakutanisha wajumbe zaidi ya 40 wanaowakilisha makundi mbalimbali ya ubia huo, wakiwemo wawakilishi kutoka nchi saba tajiri zaidi duniani (G7), pamoja na nchi washirika kutoka kanda zinazoendelea kiuchumi, hasa Afrika na Asia. Vilevile, mashirika mbalimbali ya kimataifa yanashiriki katika mjadala…

Read More

Benki ya Equity Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Mastercard imezindua kadi mpya mbili za malipo – Mastercard Gold Debit na Mastercard World Debit – katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 4 Juni 2025. Uzinduzi huo umefanyika kwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi. Akizungumza katika hafla hiyo, mhandisi Mahundi amesema kadi hizo ni sehemu ya mageuzi ya kidijitali na ujumuishwaji wa kifedha yanayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita. Amesisitiza kuwa huduma hizo mpya zitawawezesha Watanzania kupata huduma za kifedha salama, za kisasa, na zenye uwazi, hivyo kuongeza ushiriki wao katika…

Read More