Browsing: Video Mpya

Watu watatu wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa, kufuatia ajali iliyohusisha magari mawili, likiwemo Basi la abiria Kampuni ya CRN na Toyota Land Cruiser mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, katika eneo la Ilongo Wilaya ya
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Humo, Wilbat Siwa, amesema Basi lilikuwa likitokea Mbeya kuelekea Mbarali na Toyota Land Cruiser lilikuwa likitokea Njombe kuelekea Mbeya Mijini na kwamba chanzo cha ajali ni basi la Abiria ‘Ku ovateki vibaya, ambapo dereva wa basi hilo

Wananchi wa Kata ya Itewe, wilayani Chunya, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika ujenzi wa daraja jipya ambalo limeboresha miundombinu na kurahisisha usafiri katika eneo hilo. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Juma Zuberi Homera, amepongeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa mradi huo muhimu kwa maendeleo ya wananchi.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (Mbeya UWSA), kupitia Mwenyekiti wa Bodi yake, Bi. Edna Mwaigomole, imekabidhi tenki la maji lenye ujazo wa lita 5,000 kwa Shule ya Sekondari ya Wanawake Tulia, iliyopo Iyunga, Jijini Mbeya.

Hatua hii imekuja baada ya shule hiyo kuwasilisha ombi la msaada wa maji, na mamlaka hiyo kusikia kilio chao. Utoaji wa tenki hilo unalenga kuboresha upatikanaji wa maji safi shuleni hapo, hivyo kusaidia mazingira bora ya kujifunza kwa wanafunzi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Bi. Mwaigomole alisisitiza dhamira ya Mbeya UWSA ya kuendelea kushirikiana na jamii katika kuhakikisha huduma bora za maji zinapatikana kwa taasisi mbalimbali, hususan shule.

Uongozi wa shule hiyo umeishukuru Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya kwa msaada huo muhimu, wakibainisha kuwa utapunguza changamoto ya maji na kuboresha afya na ustawi wa wanafunzi.