Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- Mbunge Masache: “Rais Samia ameboresha huduma za Afya na Elimu;Mitano tena kwake!!”
- “Wakulima Festival 2025: Tamasha Kubwa la Kilimo Kufanyika Mbeya kwa Ushirikiano wa Taasisi 100
- CHAKAMWATA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI CWT NA WAKURUGENZI
- JK AWASILISHA UJUMBE WA RAIS SAMIA KWA RAIS MUSEVENI WA UGANDA LEO JIJINI KAMPALA
- Spika wa Bunge la Tanzania aongoza Waombolezaji kutoa Rambirambi kwa Kifo cha Katibu wa Bunge la Zambia
- RAIS SAMIA AUNGWA MKONO NA WATUMISHI WA AFYA KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
- CHAUMMA YATANGAZA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025
- Tulia Trust yaendelea kutoa tabasamu kwa kujenga nyumba tatu katika kata za Itezi, Uyole na Igawilo
Browsing: Video Mpya
#mbeyayetutv
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera ameagiza kukamatwa na kichunguzwa viongozi wa chama kikuu cha ushirika wilayani Kyela (KYECU) Kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kupelekea upotevu wa zaidi ya millioni 440 za wakulima, baada ya magunia zaidi ya 200 kutoonekana baada ya mnada namba tatu wa zao la cocoa uliofanyika jumatatu July 15 wilayani humo.
Pamoja na kukamatwa viongozi hao akiwemo mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilayani Kyela (KYECU) Evance Mwaipopo pamoja na Meneja wa chama hicho Julius Mwankenja, Homera ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya, kuchunguza chama hicho mifumo yao ya kifedha huku akisitisha taratibu zote za manunuzi Hadi pale kamati ya ulinzi na usalama itakapo jiridhiaha.
Awali akiwasilisha taarifa Kwa mkuu wa Mkoa, mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe Josephine Manasi, amesema hasara hiyo imeonekana baada ya mnunuzi aliyeshinda mnada namba tatu kubaini magunia zaidi ya 200 hayopo kwenye maghara kati ya magunia 1,915 yaliyoshindanishwa kwenye mnada huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamini Kuzaga kumsaka na kumkamata Kijana anayepatikana Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Kwa Kosa la Kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Maneno Makali na Kisha kuichoma moto Picha inayomuonyesha Mh:Rais.
RC Homera amelaani vikali Kitendo hicho kuwa si Cha Maadili Wala Uungwana na Kiko tofauti na Utamaduni halisi wa Wananchi Mkoani Mbeya.
Hata hivyo ametoa Masaa 24 kwa Kamanda Kuzaga Kumkamata Kijana huyo ili alisaidie Jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo na Mashambulizi hayo ambayo kayaelekeza Moja kwa Moja kwa Mh: Rais Dkt: Samia Suluhu Hassan.
Mwisho RC Homera amewasihi Wananchi Mkoani Mbeya kutojiingiza kwenye Vitendo viovu kwa Kukashifu Viongozi Makusudi badala yake wajikite katika Utafutaji na Uchapa Kazi kwa Manufaa ya Familia zao na Tanzania kwa Ujumla.
#mbeyayetutv
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 24 Mei 2024, ametembelea Kanisa la Mtakatifu Bikira Maria lililopo Cairo nchini Misri, eneo ambalo Bikira Maria alijificha na Mtoto Yesu kufuatia tishio la Mfalme Herode kutaka kumuua Mtoto Yesu. Ziara hii inasisitiza umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuendeleza amani, umoja na kuwa na uelewa wa pamoja katika imani na utamaduni wetu.
Mashauri matatu yalizofunguliwa Mahakama ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya kwa Hati ya dharula na Aidan Msigwa dhidi ya Lucas Mbwiga Mwapenza kuhusiana na mgogoro wa Kitalu cha uchimbaji madini ya dhahabu eneo la Kisumain Kijiji cha Ifumbo Kata ya Ifumbo Wilaya ya Chunya yamepokelewa na Hakimu James Mhanusi kwa ajili ya kusikilizwa.
Hati hiyo imewasilishwa Mahakama ya Wilaya na Wakili wa kujitegemea Jacqueline Massawe kwa niaba ya Aidan Msigwa wakati Lucas Mwampenza akitetewa na Wakili Boniphace Mwabukusi akisaidiwa na Wakili Irene Mwakyusa.
Mashauri yaliyowasilishwa Mahakamani na Wakili Jacqueline Massawe kwa niaba ya Aidan Msigwa ni pamoja na kesi ya msingi ya kutaka kulimiliki eneo lake analodai kulimiliki kihalali baada ya kulinunua,shauri la pili ni kusudio la zuio la kutofanyika kwa shughuli zozote katika eneo hilo na shauri la tatu ni kuendelea na shughuli licha ya kuwepo kwa zuio la Mahakama.
Wakili Massawe amempatia Wakili Mwabukusi Hati ya dharula na nakala kuwasilishwa Mahakamani na Wakili Mwabukusi naye kuwasilisha pingamizi mbele ya Mahakama.
Baada ya kupokea nyaraka za pande zote mbili Hakimu James Mhanusi ameahirisha shauri hilo hadi mei 13,2024 Mahakama itakapoanza kuzisikiliza pande zote mbili.
Nje ya Mahakama Wakili Mwabukusi ameeleza mashauri anayodaiwa katika Mahakama hiyo kupitia Hati ya dharura kuwa ni pamoja na kesi ya msingi ya kutaka kulimiliki eneo lake analodai kulimiliki kihalali baada ya kulinunua,shauri la pili ni kusudio la zuio la kutofanyika kwa shughuli zozote katika eneo hilo na shauri la tatu ni kuendelea na shughuli licha ya kuwepo kwa zuio la Mahakama.
Mahakama pekee ndiyo inatarajiwa kuumaliza mgogoro huo ili kuleta amani katika Kata ya Ifumbo.