Browsing: Video Mpya

Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya amezindua wiki ya utafiti na ubunifu Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya.

Katika hotuba yake Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema tafiti na bunifu ndiyo nguzo kuu ya uchumi Duniani.

Amesema Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kiwe sehemu ya majibu na lazima wanachuo wajitofautishe na kada nyingine kwani soko lipo ndani na nje ya nchi.

Amesema juhudi za tafiti na bunifu Chuo Kikuu MUST kimemfanya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuvutiwa na kutoa pesa kupanua huduma Mkoa wa Rukwa.

Amewahimiza wanachuo kusoma kwa bidii ili kukitangaza Chuo ndani na nje ya nchi huku akisisitiza kauli mbiu “Nafasi ya utafiti na ubunifu katika kuimarisha kilimo” alisema Mahundi.

Amepongeza Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kwa kubuni dira za maji ambazo zinasambazwa nchini huku akihimiza bunifu katika kilimo ili waweze kujiajiri badala ya kutegemea ajira serikalini.