Browsing: Video Mpya

Mashauri matatu yalizofunguliwa Mahakama ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya kwa Hati ya dharula na Aidan Msigwa dhidi ya Lucas Mbwiga Mwapenza kuhusiana na mgogoro wa Kitalu cha uchimbaji madini ya dhahabu eneo la Kisumain Kijiji cha Ifumbo Kata ya Ifumbo Wilaya ya Chunya yamepokelewa na Hakimu James Mhanusi kwa ajili ya kusikilizwa.

Hati hiyo imewasilishwa Mahakama ya Wilaya na Wakili wa kujitegemea Jacqueline Massawe kwa niaba ya Aidan Msigwa wakati Lucas Mwampenza akitetewa na Wakili Boniphace Mwabukusi akisaidiwa na Wakili Irene Mwakyusa.

Mashauri yaliyowasilishwa Mahakamani na Wakili Jacqueline Massawe kwa niaba ya Aidan Msigwa ni pamoja na kesi ya msingi ya kutaka kulimiliki eneo lake analodai kulimiliki kihalali baada ya kulinunua,shauri la pili ni kusudio la zuio la kutofanyika kwa shughuli zozote katika eneo hilo na shauri la tatu ni kuendelea na shughuli licha ya kuwepo kwa zuio la Mahakama.

Wakili Massawe amempatia Wakili Mwabukusi Hati ya dharula na nakala kuwasilishwa Mahakamani na Wakili Mwabukusi naye kuwasilisha pingamizi mbele ya Mahakama.

Baada ya kupokea nyaraka za pande zote mbili Hakimu James Mhanusi ameahirisha shauri hilo hadi mei 13,2024 Mahakama itakapoanza kuzisikiliza pande zote mbili.

Nje ya Mahakama Wakili Mwabukusi ameeleza mashauri anayodaiwa katika Mahakama hiyo kupitia Hati ya dharura kuwa ni pamoja na kesi ya msingi ya kutaka kulimiliki eneo lake analodai kulimiliki kihalali baada ya kulinunua,shauri la pili ni kusudio la zuio la kutofanyika kwa shughuli zozote katika eneo hilo na shauri la tatu ni kuendelea na shughuli licha ya kuwepo kwa zuio la Mahakama.
Mahakama pekee ndiyo inatarajiwa kuumaliza mgogoro huo ili kuleta amani katika Kata ya Ifumbo.

Mgogoro umeibuka baina ya Lucas Mbwiga na Aidan Msigwa Wawekezaji wawili wa machimbo ya dhahabu katika Kijiji cha Ifumbo Kata ya Ifumbo Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya ambapo kila mmoja anadai kulimiliki kihalali eneo la Kisumain lililokuwa na leseni ya uchimbaji wa madini kwa jina la Daud Mwantavila ambalo linadaiwa kupangishwa kwa Lucas bila ridhaa ya familia huku Aidan Msigwa akidai kulinunua kisheria na kubadilisha umiliki wa leseni kutoka kwa Daud na kuja kwake tangu April 22,2024.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde Juma Z. Homera amefika Mlima Kawetele uliopolomoka Alfajiri ya Leo na Kusababisha Kufukiwa kwa Nyumba 20, Ng’ombe Wanne na Kuharibika kwa Miundombinu ya Shule ya Generation katika Mtaa wa Gombe Kata ya Itezi Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Akizungumza baada Kuwasili eneo la Tukio RC Homera amekanusha Uvumi unaozagaa Mtandaoni ukidai Kuna Maafa katika tukio hilo ambapo amesema zaidi ya hivyo vilivyotajwa Aya ya Kwanza hakuna Madhara mengine Wala Maafa kama inavyoripotiwa na Baadhi ya Watu.

Aidha Homera ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kufanya Tathimini juu ya Waathirika hasa wale wasio na Malazi ya Kulala wahakikishe wanapatiwa Sehemu hizo wakati huu ambao Serikali inaendelea kupambana kuhakikisha Hali inakuwa Sawa katika Maeneo hayo.

Pia amekiagiza Kitengo Cha Ardhi Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuacha kuwapimia Wananchi Viwanja eneo lenye Changamoto hasa ya Mkondo wa Maji kwa kufanya Kwao hivyo kutasababisha Matatizo kama hayo ambayo yangeweza kuzuilika.

Tukio hilo limetokea Alfajiri ya Kuamkia Leo ambapo chanzo Chake ni Mvua zinazoendelea Kunyesha Mfululizo na Matukio yanayofanana na haya yamekuwa yakitukia Mikoa Mbalimbali ikiwemo Mikoa ya Arusha na Lindi.

Watu wawili jinsi ya kike wakazi wa Kiwanja Kata ya Mbugani Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wanadaiwa kuuawa na mtoto mwingine mwenye umri wa miaka sita kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali nyumbani kwao.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa aliyeuawa ni mwalimu Herieth Lupembe wa shule ya msingi Mbugani na mwingine ni Ivon Tatizo Haonga(16) mwanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya lsenyela aliyekuwa anaishi naye.

Taarifa za mauaji hayo zilipatikana jioni machi 30,2024 baada ya mwalimu huyo kutofungua duka lake na simu yake kutopatikana pia kutoonekana kanisani wakati si kawaida yake.

Baadhi ya mashuda wamedai kuwa aliagiza bidhaa za dukani kutoka Mbeya baada ya kutoonekana bidhaa hizo ziliachwa nje ya duka lake lililopo mita hamsini kutoka nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Edith Swebe Machi 30,2024 ameshiriki katika kongamano la Pasaka la Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (UKWATA) wa Shule za Sekondari Mkoa wa Simiyu ambalo limefanyika katika shule ya Sekondari Itilima iliyopo Wilaya ya Itilima.

Kamanda Swebe alipata fursa ya kuongea na vijana hao wa UKWATA Mkoa wa Simiyu na kuwahasa kujiepusha na matumizi mabaya ya Mitandao ya kijamii kwa kuangalia picha zisizo na maadili kitendo ambacho kinaweza kusababishia madhara ya afya ya akili na badala yake watumie mitandao ya kijamii kwa lengo la kujifunza.

Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson imetoa msaada wa vyombo vya kuhubiria Msikiti wa Masjid Bi Fatma Nzovwe Jijini Mbeya.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Dkt Tulia Ackson Afisa Habari wa Taasisi hiyo Joshua Mwakanolo amesema lengo ni kutekeleza ombi la Msikiti huo kwa Mbunge ambapo waliomba vipaza sauti kwa ajili ya ibada.

Kwa niaba ya Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya msemaji wake Shekhe Ibrahim Bombo mbali ya kushukuru amewaomba waumini kumuombea dua ya heri huku akitaka vyombo hivyo vitunzwe kwa uangalifu.

Naye Hemed Kipengele kwa niaba ya Waumini ametoa neno la shukurani akimshukuru Mbunge kwa kutoa vifaa hivyo bila kujali itikadi za Kidini.

Aidha Justin Kayuni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Ndanyela ameipongeza Taasisi ya Tulia Trust kwa kutoa vifaa hivyo kwani vitasaidia kueneza neno la Mungu.

Hatimaye Abdalah Yundu Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ameongoza dua ya kumuombea Dkt Tulia Ackson katika kazi zake za kila siku.

Dkt Tulia amekuwa akitoa misaada mbalimbali bila kujali itikadi za Kidini na Kisiasa ambapo hivi karibuni amefanikisha ujenzi wa Misikiti ya Tukuyu Mjini,Kiwira Wilayani Rungwe na Uyole Jijini Mbeya.

Zaidi ya bilioni kumi na Moja zimetumika kukamilisha ujenzi wa miradi mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ndani ya miaka mitatu tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya sita kutokana na aliekuwa rais wa awamu ya Tano kufariki Dunia mwanzoni mwa mwaka 2022 Hayati Dkt.Pombe Joseph Magufuri.

Hayo yamebainishwa na Mganga mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya Dkt.Abdallah Mmbaga wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya hali ilivyo tangu Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwepo madarakani.

Baadhi ya wananchi waliopo Mkoani Mbeya wamezungumzia hali ya huduma ilivyo katika hospitali hiyo wakisema maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali yamefanya hospitali hiyo kuwa kimbilio la haraka kwao huku wakiwapongeza watumishi wa hospitali hiyo kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa tofauti na zamani.

Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya huhudumia wakazi wa Wilaya za Mbeya,Kyela,Chunya,Mbarali na Rungwe.

Jeshi la Polisi Nchini limesema Machi 20, 2024 lilitoa taarifa kuhusiana na kifo cha Omary Saimon Msamo kilichotokea huko Wilayani Karatu Mkoa wa Arusha Machi 16, 2024.

Akitoa taarifa hiyo leo machi 26,2024 Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime amesema Jeshi hilo lilieleza mazingira ya tukio hilo ambapo amebainisha kuwa ilibidi kushirikisha wataalam mbalimbali wakiwepo wachunguzi wa matukio ya vifo.

DCP Misime aliendelea kueleza kuwa Timu ya uchunguzi wa tukio hilo ilipofanya uchunguzi wa tukio hilo ilibaini kuwa kifo chake hakikuwa cha kawaida bali ilikuwa ni Mauaji.

Aidha Msemaji wa Jeshi hilo alisema Baada ya kubaini hivyo Jeshi hilo lilianza uchunguzi wa mauaji hayo ambapo lilibaini waliohusika wa mauaji hayo.

Sambamba na hilo amebainisha kuwa uchunguzi umebaini kuwa malengo yalikuwa ni kumpora Omary Saimon Masamo chochote kile watakacho mkuta nacho.

Misime ameviambia vyombo vya habari kuwa Waliohusika na mauaji hayo tayari wamekamatwa na wamekutwa wakiwa na simu ya marehemu huku fedha walizompora kiasi cha Shilingi 200,000/= wakiwa tayari wameshagawana na kuzitumia.

Waliokamatwa ni Anthony Paskali ambaye anajulikana kwa jina maarufu Lulu na Emmanuel Godwin Jeseph anayejulikana kwa jina maarufu la Emma wote wakiwa ni wakazi wa Wilaya ya Karatu.

Taratibu zilizobaki za kiuchunguzi zinakamilishwa ili hatua nyingine za kisheria ziweze kufuata.

Pia DCP Misime amesema Jeshi la Polisi linaendelea kutoa tahadhari kwa baadhi ya watu kuacha kueneza taarifa za uwongo, chuki na uzushi dhidi ya mtu mwingine au taasisi kwa ajili ya malengo yao binafsi kwani kwakufanya hivyo watakuwa wanaukaribisha mkono wa sheria uweze kuwafikia na kuchukuliwa hatua.